SGR ingekuwa Vyema Ingepita Chalinze na Kibaha

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Hii Treni ya Sgr ingepita Karibu na miji Midogo ya Mdaula, Chalinze, Mlandizi na Kibaha Ingekuwa fursa kubwa sana kiuchumi na Watu wengi wangeishi katika miji hii na kufamya shughuli zao Dar es Salaam kwa Urahisi sana Sijui kwa nini Wenye maamuzi hawakuliina hili
Hii tabia ya kupitisha treni maporini haina Afya

Pia Nimeshangazwa na Manispaa ya Morogoro Kushindwa Kutengeneza Stand ya Abiria karibu na Station ya SGR kioindi chote ambacho Miundo Mbinu ya SGR inajengwa wao walikuwa Wapi?
 
Wamekimbia fidia. Ingawa una hoja.
 
Ingepita Mbezi Mwisho ingekuwa poa sana
 
Siyo kila eneo linafaa kupitiwa na reli.

Reli inataka eneo tambarare lisilo na milima. Hicho ndicho kigezo Cha kwanza.

Hata hivyo reli ya SGR imepitia Wilaya ya Kisarawe Kata ya Kazimzumbwi na Mzenga. Huko ardhi ni bei Chee, hivyo unaweza kwenda kuwekeza huko.
 
Mkuu comment yako naifanyia kazi, shukrani!
 
Nasikia kuna tycoon anataka kujenga apartments Ruvu na Soga
 
Mtu kama huyu unakuta nae anasimama anasema viongozi hawana akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…