Kyara Atufigwe
Senior Member
- Mar 29, 2015
- 120
- 68
SGR ni ufupisho wa maneno ya lugha ya kiingereza ambayo ni Standard Gauge Railway. Hii ni reli ya kisasa ambayo ina upana wa sentimeta 1,435, inayotumika katika mataifa mengi duniani kwa zaidi ya 55% na kuachana na mfumo uliopitwa na wakati wa reli ya geji ya mita moja (One Meter gauge). Reli hii ya kisasa ya SGR ina uwezo mkubwa zaidi wa kusafirisha uzito mkubwa na kwa kasi kubwa zaidi kuliko reli ya kawaida. Reli hii ya kisasa ni ya kwanza Afrika Mashariki itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nishati ya Umeme na yenye mwendokasi usiopungua Kilometa 160 kwa saa kwa treni ya abiria, na Kilometa 120 kwa saa kwa zile treni za mizigo.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Reli Tanzania (T.R.C) limeanza kujenga reli hii ya kisasa. Mradi wa ujenzi wa reli hii ya kisasa umegawanywa katika awamu kuu mbili ambapo kila awamu ina vipande tofauti tofauti. Awamu ya kwanza inahusisha Ujenzi wa reli ya SGR kutoka Dar es salaam hadi Mwanza. Awamu hii imegawanywa katika vipande vitano (5) ambapo vipande hivi vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake.
Awamu ya pili ya ujenzi wa reli hii utahusisha Tabora hadi Kigoma, Uvinza - Msongati - Gitega hadi Kindu (Kongo J.K) na Kaliua – Mpanda hadi Bandarini Karema. Mtandao wa reli ya kisasa kwa awamu ya kwanza ambao ukikamilika utakuwa na urefu wa Km 2,561; utaunganisha mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Kigoma, Katavi na Mataifa jirani kama vile Kongo J.K, Rwanda, Burundi na Uganda.
Aidha, ujenzi wa reli hii ya kisasa yenye mtandao wa kilometa 1,219 za njia kuu kwa awamu ya kwanza ya Dar es salaam hadi Mwanza, umegawanywa katika vipande vitano; ambavyo ni Dar es salaam hadi Morogoro (Km 300), Morogoro hadi Makutupora (Km 422), Makutupora hadi Tabora (Km 368), Tabora hadi Isaka (Km 165) na Isaka hadi Mwanza (Km 341)
Kipande cha kwanza cha Dar es salaam hadi Morogoro, ujenzi wa reli na miundombinu ya umeme umeshakamilika kwa 100%; Kwa sasa kazi kubwa inyoendelea ni majaribio ya mifumo mbalimbali ya umeme (Power system energization) na kazi inaendelea vizuri sana.
Aidha, kipande cha pili cha Morogoro hadi Makutupora kimekamilika kwa zaidi ya 90%, ujenzi unaendelea vizuri sana, Makutupora hadi Tabora ujenzi unaendelea baada ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kushuhudia utiwaji saini wa Ujenzi wa kipande hiki mwezi Aprili 2022. Aidha, Kampuni ya Yapi Merkez inaendelea na ujenzi wa kipande cha Tabora hadi Isaka, ambapo sasa ujenzi umefikia 10%; na kipande cha tano cha Isaka Mwanza ujenzi tayari upo kwenye hatua mbalimbali.
Sambamba na hayo, Mhe Rais aliahidi pia ujenzi wa awamu ya pili yenye kilometa 1,010 itakayohusisha vipande vipya vya Tabora hadi Kigoma (Km 411), Uvinza – Msongati - Gitega hadi Kindu (Kongo J.K) (Km 282) kwa ushirikiano na Serikali za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo; na baadaye kipande cha Kaliua – Mpanda hadi Karema.
Ujenzi huu wa mtandao wa SGR una maana gani kwa uchumi wa Taifa letu? Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa SGR kutoka Dar es salaam hadi Mwanza kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwenda nchi jirani za Kongo J.K, Rwanda, Burundi na Uganda na hivyo kukuza maradufu sekta ya Biashara na usafirishaji nchini. Aidha, mizigo bandarini itasafirishwa kwa haraka sana na hivyo kupunguza mrundikano wa mizigo katika bandari ya Dar es salaam. Hali hii itazidi kuchochea mapato ya nchi.
Aidha, mizigo itakayosafirishwa kupitia bandari ya Dar es salaam itaongezeka maradufu kutokana na urahisi na unafuu wa gharama za usafirishaji. Imebainishwa kuwa gharama za usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli ni nafuu zaidi kwa mfanyabiashara kuliko usafirishaji kwa njia ya barabara. Unafuu huu wa gharama za usafiri utazidi kuchochea zaidi biashara ndani na nje ya nchi. Ni matarajio ya wengi kuwa Wafanyabiashara wa Mataifa ya Kongo J.K, Rwanda, Burundi, Uganda na hata Sudani ya Kusini watajikita kutumia bandari ya Dar es salaam.
Pia, kukamilika kwa awamu ya kwanza ya SGR ya Dar es salaam hadi Mwanza kutaiunganisha Bandari ya Dar es salaam na wafanyabiashara wa Taifa la Sudani ya Kusini kupitia bandari ya Bell (Port Bell) nchini Uganda na hivyo kupanua wigo wa biashara nchini. Kibiashara, Wafanyabiashara wa Sekta ya Usafirishaji nchini Uganda wataifurahia sana fursa hii kuliko Mizigo ya Sudani Kusini kupitia bandari ya Mombasa nchini Kenya; kwani fursa ya kusafirisha mizigo kutoka Port Bell hadi Juba na sehemu nyinginezo nchini humo itakuwa mikononi mwao.
Aidha, kutokana na ufanisi wa treni za umeme, mizigo itasafirishwa kutoka Bandari ya Dar es salaam hadi nchini Uganda ndani ya siku moja, hivyo kuifanya bandari hiyo ivutie zaidi kuliko bandari shindani ya Mombasa. Hivyo basi, bandari ya Dar es salaam ijipange kupokea mara tano ya shehena inayopokea sasa. Hatua hii itakuza sana Uchumi wa Taifa letu.
Mradi huu wa SGR umeongeza sana ajira nchini. Vijana zaidi ya 10,000 wamepata ajira na kukuza vipato vyao; hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa letu. Aidha, wakandarasi wazawa wamepata fursa ya kushiriki moja kwa moja kutoa huduma ambapo takribani wazabuni 500 wanashiriki, kati yao 15 ni Kandarasi za kati kwenye ujenzi wa SGR na hivyo kujifunza ujuzi ambao haukuwepo mwanzoni katika Sekta ya Ujenzi nchini.
Aidha, katika hatua hizi za utekelezaji wake, SGR imekuza sana sekta ya viwanda nchini kwani mahitaji ya Saruji, nondo na vifaa mbalimbali vya ujenzi yameongezeka maradufu, hivyo kuvifanya viwanda vya ndani kupata soko kubwa na la uhakika na hatimaye kuzidi kuchangia pato la Taifa. Mathalani, kwa kipande cha Dar es salaam hadi Morogoro tu kiasi cha nondo kilo milioni 45 za kiwango cha BS 500 pamoja na mifuko ya saruji takribani milioni 3 vimetumika. Vifaa hivi vyote vimezalishwa na viwanda vya ndani.
Mradi wa SGR pia umetoa fursa kwa wafanyabiashara wa Sekta ya Usafirishaji nchini. Baadhi yao wamekodisha magari yao pamoja na kushiriki moja kwa moja katika kusafirisha vifaa na mitambo mbalimbali. Hali hii imechochea sana ukuaji wa kipato cha mwananchi na Pato la Taifa kwa Ujumla.
Kwa kuwa treni yetu itatumia Umeme badala ya mafuta, mradi huu utaongeza soko la ndani na hivyo kuimarisha thamani ya Shilingi ya Tanzania. Kwa kuepuka matumizi ya diesel, tumezidi kuimarisha akiba ya fedha za kigeni na kupunguza gharama kwa nchi.
Pia, kutakuwa na ongezeko kubwa la usafirishaji wa mizigo ambapo inakadiriwa kuwa reli itakuwa na uwezo wa kubeba mizigo hadi tani 10,000 sawa na malori 500 kwa njia ya barabara. Katika hili pia, Serikali itaimarisha akiba ya fedha za kigeni kwa kuepuka gharama za kujenga upya na kukarabati barabara za lami mara kwa mara kutokana na uharibifu ambao umekuwa ukifanywa na malori yanayobeba tani nyingi za mizigo kwa umbali mrefu.
SGR pia itachochea ukuaji wa sekta za kilimo, biashara na viwanda hususani maeneo ambapo reli itapita, pamoja na nchi jirani za Rwanda, Burundi, Kongo J.K, Uganda na Sudani ya Kusini. Wananchi wa maeneo kama Kilosa, Dodoma, Manyoni, Tabora, Mwanza, Kigoma na Mpanda watapata fursa ya kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za nafaka, mafuta ya kula, karanga, asali, Pamba, mifugo n.k na bidhaa nyingine za viwandani na hivyo kukuza vipato vyao na Pato la Taifa kwa ujumla.
Aidha, SGR inatarajiwa kupunguza gharama na muda wa kusafirisha bidhaa na abiria kwenda maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Mathalani, safari ya Dar es salaam hadi Morogoro itachukua saa 1 na dakika 15 badala ya zaidi ya masaa manne(4) ya sasa; Dar es salaam hadi Dodoma itakuwa ni safari ya masaa matatu (3) badala ya masaa zaidi ya nane (8) ya sasa. Aidha, gharama za usafirishaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es salaam inatarajiwa kushuka kwa 40% na hivyo kuifanya Bandari ya Dar es salaam ivutie zaidi katika ukanda huu kuliko bandari shindani ya Mombasa.
Pia, Mradi huu wa SGR unatarajiwa kuwa na matokeo mengi chanya kwa vijiji na miji mbalimbali nchini. Vijiji kama Soga, Ruvu na Kwala kwa Mkoa wa Pwani vinatarajiwa kukua kwa kasi na kuwa miji kutokana na kuwa na vituo muhimu vya treni ambapo biashara zinatarajiwa kukua na kuimarika zaidi, hivyo kuchochea ukuaji wa kipato cha mwananchi wa kawaida na Pato la Taifa kwa ujumla.
Kwa ujumla, kukamilika kwa Mradi wa Ujenzi wa reli ya Kisasa ya SGR nchini ni ukombozi mkubwa kwa uchumi wa Taifa letu. Tanzania itavutia zaidi kibiashara na kuifanya kuwa kitovu cha biashara katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki. Ni vema sasa Bandari ya Dar es salaam na watanzania kwa ujumla tuchangamkie fursa hii na kujipanga kuhudumia wafanyabiashara wa zaidi ya nchi tano kupitia mtandao wa reli hii ya SGR. Taifa litakusanya fedha nyingi kupitia bandari na biashara zitakazochochewa na mazingira hayo mazuri na rafiki kibiashara nchin