SGR zihurumieni kodi zetu

SGR zihurumieni kodi zetu

Kalunya

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2021
Posts
13,322
Reaction score
18,609
Wasalamu sioni haja ya kujenga madaraja vivuko vya magari kwenye mapitio ya magari wakati kuna njia mbadala na nafuu kwanini msiinue reli kwa kuongeza ukubwa wa tuta treni ipite juu magari yapite chini kupunguza gharama kama mfano wa karavati kubwa gari zipite chini.

Airport mbomoe nyumba mjenge daraja mmeua uchumi wa pembeni mwa barabara Yale maduka yanategemea watu na magari yapitayo pale, pili ni shortcut ya kuchepuka kwa watakaopita njia ya vumbi kuelekea banana na kinyerezi. Buguruni na Gongo la Mboto mmeinua hizi cross zingine ikiwemo hii ya airport ni kubwa kwanini msiinue tuta kuliko kujenga fly over gharama yote ya nini, daraja lianze kwenye mataa hadi kuvuka FQ hotel karibu kilometa moja ya nini.

Kwanini msiinue tuta la kifusi toka Kipawa hadi Banana Ili kwenye maungio yote magari yapite chini ni gharama nafuu zaidi kuliko kujenga fly over kwenye maungio. Au kwanini msiweke mageti ya umeme na walinzi kama ilivyo ulaya na kwani hio treni itakuwa inapita kila dakika hadi mlazimike kujenga maflyover, hamuoni mtaathiri watumiaji wengine wa barabara? Kama ni speed iwe maporini na sio mijini maana still vivuko visivyo rasmi ni vingi kwa waenda kwa miguu.Pia watu wanahitaji huduma za haraka mfano dharura au ugonjwa yaani uende ukafate kivuko kilometa 2 ndipo urudi position yako ya awali.

Wakati mnafanya project mpende kuwashirikisha na watuamiaji wengine si reli tu ndo wenye haki zote za kutumia ardhi.watu,magari, pikipiki, baiskeli nk navyo vinayo haki SAwa ya kutumia ardhi. Economic of scale na others users haikuzingatiwa kwenye upembuzi uaminifu. Nawasilisha.

MAJIBU
 
Saa nyingine kupenda vitu rahisi kuna leta matatizo.

Hayo matuta yako yanaweza kusababisha mafuriko baadhi ya sehemu. Eg. Mfugale Tazara Flyover kuna ukuta mfano wa tuta lililoleta mafuriko wakati Ubungo Exchange hakuna tuta kuna nguzo hakuna mafuriko.

Kuleta usumbufu kwa njia za mitaani.

Kwenye makazi ya watu wengi rahisi watu kujaribu kupanda tuta wakapata ajali.

Muonekano mbaya wa mandhari ya mji.
 
Hio gharama za kujenga flyover toka mataa airport kupita Hotel za FQ kama kilometa moja kasoro hivi zingepungua kama mngeinua tuta la kifusi toka kipawa hadi banana.
 
Mafuriko ya nn ukijenga mifereji na matoleo ya maji pande zote?
 
Kwanini msiinue tuta la kifusi toka Kipawa hadi Banana Ili kwenye maungio yote magari yapite chini ni gharama nafuu zaidi kuliko kujenga fly over kwenye maungio
Picha mkuu ili nasi tuchangie hoja
 
Picha mkuu ili nasi tuchangie hoja
Sina picha lakini maliasili gongolamboto jirani na kiwanda cha nguo kuna karavati kubwa kama daraja hata gari kubwa linapita.
 
Mzee ile reli kwa ajiri ya treni ya umeme ambazo zinakimbia kama Ferrari, ukiinua inua ovyo kila sehemu inaweza kupaa kama ndege
Mbio zianzie pugu na sio mjini still vivuko visivyo rasmi ni vingi pili itakuwa inapita KILA sekunde?Maana ratiba za treni ujulikana.
Mjini kwa mwendo wa ferari biashara ya majeneza italipa Sana.
Kila sehemu wakiweka flyover hadi pugu si gharama kubwa
 
Kizuri ngarama wewe unataka matuta tena kwanza mjini
 
Wasalamu sioni haja ya kujenga madaraja vivuko vya magari kwenye mapitio ya magari wakati kuna njia mbadala na nafuu kwanini msiinue reli kwa kuongeza ukubwa wa tuta treni ipite juu magari yapite chini kupunguza gharama kama mfano wa karavati kubwa gari zipite chini.

Airport mbomoe nyumba mjenge daraja mmeua uchumi wa pembeni mwa barabara Yale maduka yanategemea watu na magari yapitayo pale, pili ni shortcut ya kuchepuka kwa watakaopita njia ya vumbi kuelekea banana na kinyerezi. Buguruni na Gongo la Mboto mmeinua hizi cross zingine ikiwemo hii ya airport ni kubwa kwanini msiinue tuta kuliko kujenga fly over gharama yote ya nini, daraja lianze kwenye mataa hadi kuvuka FQ hotel karibu kilometa moja ya nini.

Kwanini msiinue tuta la kifusi toka Kipawa hadi Banana Ili kwenye maungio yote magari yapite chini ni gharama nafuu zaidi kuliko kujenga fly over kwenye maungio. Au kwanini msiweke mageti ya umeme na walinzi kama ilivyo ulaya na kwani hio treni itakuwa inapita kila dakika hadi mlazimike kujenga maflyover, hamuoni mtaathiri watumiaji wengine wa barabara? Kama ni speed iwe maporini na sio mijini maana still vivuko visivyo rasmi ni vingi kwa waenda kwa miguu.Pia watu wanahitaji huduma za haraka mfano dharura au ugonjwa yaani uende ukafate kivuko kilometa 2 ndipo urudi position yako ya awali.

Wakati mnafanya project mpende kuwashirikisha na watuamiaji wengine si reli tu ndo wenye haki zote za kutumia ardhi.watu,magari, pikipiki, baiskeli nk navyo vinayo haki SAwa ya kutumia ardhi. Economic of scale na others users haikuzingatiwa kwenye upembuzi uaminifu. Nawasilisha.

MAJIBU
Sidhani kama una utaalamu wowote kwenye fani za uhandisi..unadhani ww ndo una akili nyingi sana wataalamu hawakuliona hilo..Heshimu utaalamu wa watu kwani huo mradi kitaalamu unaangalia mambo mengi sana kuliko unavyofikiria.
 
Sioni kama shida ni wataalamu kufikiria tatz nchi yetu upigaji ndio unapewa kipaumbele
Pic%20Layer_202111923101073.jpg
 
Hio gharama za kujenga flyover toka mataa airport kupita Hotel za FQ kama kilometa moja kasoro hivi zingepungua kama mngeinua tuta la kifusi toka kipawa hadi banana.
Mkuu acha watu wajenge... Vitu vya bei chee sio vizuri sana hasa kwa mda mrefu ujao.
 
Sidhani kama una utaalamu wowote kwenye fani za uhandisi..unadhani ww ndo una akili nyingi sana wataalamu hawakuliona hilo..Heshimu utaalamu wa watu kwani huo mradi kitaalamu unaangalia mambo mengi sana kuliko unavyofikiria.
Kuwa mtaalamu hakumaanishi ndo kujua kila kitu.
 
Lengo ni kuwa na miji ya kisasa. Huenda idea yako haikubaliki katika kufikia lengo hilo. Labda uweke picha za majiji ya kisasa yaliyotumia hiyo system yako.
 
wewe ni mtaalam au ndio ile Mtanzania ni Injinia, Mbea, Usalama, Mwalimu

Wakati mwingine punguza ujuaji dogo . Sgr sio jiko hilo ndg
 
Mbona wameinua sehemu zingine
 
wewe ni mtaalam au ndio ile Mtanzania ni Injinia, Mbea, Usalama, Mwalimu

Wakati mwingine punguza ujuaji dogo . Sgr sio jiko hilo ndg
Bwana mifugo amjui ng'ombe zaidi kuliko mfugaji,afisa samaki amjui samaki kuliko mvuvi.
Wataalamu wangejua KILA kitu kodi zetu zisingetumika hovyo pasipotija.
Wangejua KILA kitu wasingejenga ofisi za mwendokasi kwenye mkondo wa maji jangwani.
Nadharia ya kujua kila kitu ndo imetufanya tusiendelee.
 
Ukute ulisoma HKL lakini kwasababu uko Jamii forum na wewe ni mtaalamu wa Civil engineering au architecture

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom