Sumasuma
JF-Expert Member
- Jun 23, 2011
- 342
- 110
Gasper Andrew, Singida
HOSPITALI Teule ya Wilaya ya Singida ya Makiungu, imetumia zaidi ya Sh1.2 bilioni kugharimia ujenzi wa hosteli ya kisasa na upanuzi wa wodi ya wazazi. Hayo yalielezwa juzi na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Maria Borda, wakati akitoa taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone, muda mfupi baada ya mkuu huyo kuyafungua majengo hayo.
Alisema Sh529.2 milioni zilitumika katika upanuzi na ukarabati wa wodi ya wazazi, lengo likiwa ni kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezeka siku hadi siku. Dk Borda alisema, wamekuwa wakitoa elimu kwa wajawazito juu ya uzazi salama na hatua hiyo imesababisha ongezeko kubwa la wanawake hao kukimbilia kujifungua hospitalini hapo.
Hali hii imesababisha msongamano mkubwa wa wajawazito katika wodi iliyopo, hivyo wengi wao hulazimika kutandika magodoro sakafuni kwa kukosa vitanda. Hali hii imesababisha hitaji la kukarabati na kupanua zaidi wodi ya wazazi ambao wanatibiwa bure", alisema.
Aidha, mganga huyo alisema wametumia Sh682.8 milioni kugharimia ujenzi wa hosteli ya kisasa ya ghorofa mbili, kwa ajili ya watumishi na wageni mbalimbali, wanaotembelea hospitali hiyo. Mradi huu wa hosteli ulibuniwa kutokana uhaba mkubwa wa nyumba za kuishi watumishi wa kada za juu pamoja na wataalamu wengi wa kujitolea, wanaokuja kila mwaka kusaidia katika fani mbalimbali, alifafanua Dk Borda.
Dk Borda alitumia fursa hiyo kuwashukuru na kuwapongeza wafadhili waliosaidia kufanikisha ujenzi huo ambao ni Maltesa Mission Fund na Cork,Singida Partinership kwa upande wa hosteli.Pia Shirika la Cordaid kupitia Stichting Makiungu la nchini Holland, Maltese Mission fund na Ubalozi wa Nigeria nchini kwa upande wa upanuzi na ukarabati wa wodi ya wazazi. Hospitali ya Makiungu ilianzishwa mwaka 1954 na masista wa Kanisa la Katoliki kwa sasa inaendeshwa kwa ubia na Halmashauri ya Wilaya ya Singida.:A S 465: