Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,752
- 5,609
HATA LUAMBO ALIIMBA
Naam, Shaaban Dede ni Mwanamuziki wa Dansi aloacha alama kupitia kazi nyingi kwenye ulimwengu wa Dansi, Mungu ampe kauli thabiti huko aliko [emoji24][emoji24].
Mimi nimsikilizapo bwana huyo kupitia tungo zake ama kazi zake sioni nongwa wala hiana kwamba kwa uwezo wa kutunga gwiji huyo alizidiwa na Marijani Rajabu pekee, sijamsikia mwingine, wapo lakini Kwa "levo" ile bado.
Binafsi ni mtumwa wa matumizi ya Lugha fasaha yenye ujazo wa tamathali za semi ni kwa mintarafu hiyo namuona bwana kwamba alitimia.
Waweza maizi (baini) kupitia tungo zake kadhaa, mfano Shangwe ya harusi huko utakutana na maneno kama "Bomu la simanzi".
Ama kupitia kibao Aziza, waweza uona mpangilio wa maneno kama vile; "pokea wangu waraka Kipenzi wa imani nimekuchagua wewe huna mshindani Aziza mboni ya jicho langu....."
Ama kama haitoshi gwiji huyu anasikika pahala akighani;
".........hubabaika na kujisachi nilicho nacho bila wewe kuniomba ....."
Ni safari ndefu kumsawiri fundi huyu, lakini kama haitoshi mwamba huyu alijaaliwa uwezo mkubwa wa kutumia maneno ambayo kwayo "angeicha kwenye mataa hadhira".
Waweza msikiza ( msikiliza ) kupitia kupitia vibao talaka rejea akiwa DDC Mlimani Park na pia Suluhu alipohamia Msondo Ngoma akitokea Mlimani Park Orchestra [emoji2][emoji2][emoji2099][emoji2099].
Luambo na Sam Mangwana waliimba Kibao kiitwacho Toujors, maudhui ya wimbo yanabebwa na maneno "Muongo na Mulozi ni watu wa kuchoma".
Neno Mulozi si muhali kulibatiza mchawi, sijui nini kiliwakuta mafahari hawa mpaka wakaungurumisha kibao hicho [emoji2099][emoji2099][emoji2099].
Bingwa huyo Shaaban Dede Kamchape "Super Motisha" akiwa na Bendi ya Mlimani Park Orchestra, walitoa kibao kiitwacho "Acha Umbea".
Ujenzi wa kisa umejikita katika maneno machache lakini yanasindikizwa kwa ustadi wa kiwango cha juu kabisa na mpigaji wa gitaa Ongozi Ramadhani Mapesa, ala za upepo na Super Konga Ally Jamwaka wameifanya kazi iliyotukuka katika wimbo huo.
Wakiongozwa na Shaaban Dede, wanasikika wakiimba [emoji1541];
"Acha umbea we Mwana
We Mwana umbea utakuponza
Ushambenga utakuponza
Uongo utakuponza
Utapatwa na aibu utakaposutwaa
Nasema acha mambo hayo nasema heeee
Acha mambo hayo nasema ooooh
Achana na umbea
Nasema
Si vizuri ndugu
Epuka we bwana
Nasema........." (nitauweka hapa uusikilize mwenyewe)
Tabia za uongo, umbea, ushambenga, kimbelembele hazijawahi kuiacha jamii katika usalama abadani, ndiyo maana ikasemwa "ulimi kiungo kidogo lakini matatizo yake makubwa".
Kwa nafasi hii, kupitia kupitia wimbo huu, Shaaban Dede kupitia Bendi ya Mlimani Park Orchestra, alivaa viatu vya Walimu katika Jamii
Niseme "Marahaba" Ramadhani Mapesa "solo dola" [emoji1547][emoji1547]
Kwa kazi uliyoifanya humo ndani ya kibao hicho [emoji3449][emoji3449]