wakati utafika MLACHA atatoka kama alivyoingia, naye analijua hilo, wala hategemei kuwa ataishi katika post hiyo milele, atakuja PFA mwingine na yeye mlacha atabaki kuwa mlacha, na waosha vinywa watatafuta mengine ya kuongea!
kwa nchi ya tanzania ambayo kila mtu anakwamisha uwajibika wa mwenzie matatizo hayo hayawezi kukosekana, labda niulize hivi huko mkwawa, duce, katika halmashauri na kurugenzi ambako kila mtu analia kwa kukosa haki yake nako ni mlacha anakwamisha, hivi ni walimu wangapi either ndani ya miaka mitano hii au nyuma zaidi ya hapo wamekuwa wakidai na wanadai pesa zao za mishahara ambazo hazina hazijawalipa, ni walimu wangapi ambao wanatolewa katika payrol za hazina huku halmashauri husika zikiwa hazijui kwanini wametolewa wanashangaa tu mishahara yao haiji, je haya nayo ni ya MLACHA, nadhani tunaangalia tulipoanguka sio tulipojikwa, suala la malipo ya wanafunzi ipo board husika na baaadhi ya pesa wala haziingi chuo ni direct payment kwa wanafunzi nalo hilo pia ni MLACHA, ama kweli ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya!