TANZIA Shabiki aliyeandika mabao yote ya Messi katika makaratasi afariki dunia

TANZIA Shabiki aliyeandika mabao yote ya Messi katika makaratasi afariki dunia

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Hernan Mastrangelo ambaye alijulikana zaidi kwa jina la Don Hernandied amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 101, huyu anasifika kuwa shabiki wa Lionel Messi ambaye aliandika katika makaratasi mabao yote ambayo yalifungwa na mchezaji huyo.

Mjukuu wa mzee huyo, Julián ndiye ambaye alianza kufichua siri kwa kuandika kuwa babu yake ni shabiki mkubwa wa Messi na amekuwa akiandika takwimu za mabao ya mshambuliaji huyo wa PSG, tangu aanze kucheza soka la kulipwa.

“Amekuwa akiandika asisti ilipotoka, dakika, mechi na tarehe ya mchezo ambao amefunga. Alikuwa akifanya hivyo kwa kuandika katika makaratasi,” alisema mjukuu huyo.

Don Hernán alifikwa na umauti juzi, hadi sasa Messi hajajitokeza hadharani kulizungumzia hilo.

FK7Ep5FaMA08bn9.jpg
 
Back
Top Bottom