Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,258
Huenda sasa ndiyo wakati wa Yanga kuonyesha upendo kwa mwenzao kwa kuwa shabiki na Mwanachama wa Klabu ya hiyo, Carlos Leonald ‘Carlos The Don', ni mgonjwa na anasumbuliwa na miguu.
Taarifa zinaeleza ni ugonjwa ambao ameupata siku chache baada ya timu yake kutoka Mbeya ilipoenda kucheza na Mbeya City, mwezi uliopita.
Carlos ambaye katika michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyopita kisiwani Zanzibar, alijulikana baada ya kuingia uwanjani na kutoa glavu za kipa wa Shaba wakati mechi ikiendelea kwenye Uwanja wa Amaan, kisha kukimbia nazo, amezungumza na gazeti hili na kufafanua juu ya kinachomsumbua.
"Hali yangu ni mbaya, kuna wakati nahisi mwili unapooza, nimejaribu kuzunguka kutafuta tiba lakini mambo yamekuwa magumu, nimekuwa mtu wa kusaidiwa kila kitu, sijapata msaada wa kuniwezesha kurudi katika hali yangu ya kawaida.
"Huu si ugonjwa wa kawaida nahisi hapa kuna namna yoyote imefanyika mpaka mimi kuwa kwenye hali hii," alisema.
Wakati huohuo, alipozungumza na mwandishi mwingine wa gazeti hili, alisema anaendelea vizuri na hajajua nini hasa kinachomsumbua lakini kuna wakati anajaribu kusimama lakini hawezi kutembea kwa umbali mrefu.
chanzo ni blog ya Saleh Jembe