TANZIA Shabiki kindakindani wa Yanga, Rebeca Miyeye afariki dunia Wilayani Sikonge

TANZIA Shabiki kindakindani wa Yanga, Rebeca Miyeye afariki dunia Wilayani Sikonge

ANCIENT FROM EGYPT

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2015
Posts
927
Reaction score
1,136
Tawi la WanaYanga Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora Wameondokewa na shabiki wao aliyekuwa na mapenzi ya dhati na Timu ya Yanga ambaye alifarikia siku ya jana katika ajali ya basi iliyotokea wilayani Sikonge.

Mwanamama huyo aliyefahamika na wengi kwa jina la Rebeca Miyeye, alikuwa shabiki kindakindaki wa Timu ya Yanga wilayani Sikonge na Tabora Kwa ujumla.

Enzi za uhai wake Bi Rebeca alifahamika kama shabiki wa Yanga mwenye mbwembwe nyingi sana hasa pale anapokutana na watani wa jadi. Na ndipo watu walipompa jina la "Mama Wa Yanga"

Natoa pole kwa familia pamoja na ndugu na jamaa waliofikwa na Msiba Huo.

NB: Samahani sana, Sina habari Za Kina juu ya Ajali hiyo ya Basi ambayo ilitokea jana.

3d202171-c4f8-4c1a-af23-824882dd6073.jpg
 
Huyo Feitoto si mtu wa bara ehee!Maana huto tumacho kwa mashababi,R.I.P mama Yanga.Pengo umeliacha.
 
Back
Top Bottom