Shaffih Dauda & Co. acheni uzandiki wenu wa kuiandama Yanga.....

Shaffih Dauda & Co. acheni uzandiki wenu wa kuiandama Yanga.....

Balantanda

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2008
Posts
12,480
Reaction score
4,775
Kwa muda mrefu sasa nimeshangazwa na propaganda chafu zinazoenezwa na Shaffih Dauda kupitia blog yake pamoja na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM dhidi ya timu ya Yanga.....Shaffih na wenzake akina Ibrahim Masoud ''Maestro'(ambaye ni kiongozi wa watani zetu Simba) kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiisakama Yanga kupitia blog hiyo na Redio kiasi cha kusema kwamba Yanga inakufa sasa.....

Nataka tu kumwambia Shaffi na wenzake Maestro,Jeff Leya na Alex(Luambano) kwamba pamoja na uzishi na fitna zao Yanga kamwe haitakufa,kutokufanya vizuri mwaka huu si kigezo cha kuitabiria kifo Yanga na akumbuke kwamba Yanga sasa hivi iashika nafasi ya 3 na si ya mwisho wala ya 2 ama 3 kutoka mwishoni sasa iweje awaalike akina Mwaisabula na kuanza kuitabiria Yanga kifo?.....Yanga imeanzishwa mwaka 1935 na bado ipo na itaendelea kuwepo......

Ni upuuzi kuisakama timu ambayo inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi na ambayo bado inaweza hata kushika nafasi ya 2......Msimu wa mwaka 1989 Simba iliponea chupuchupu kushuka daraja katika ligi daraja la kwanza lakini hakuna mtu aliyeitabiria Simba kifo.......Chuki binafsi hazijengi,zinabomoa...

Shaffih na Clouds wanaweza kufanya mambo mengi tu mengine badala ya kutwa kucha kuisakama Yanga kwa sababu tu imepoteza mechi 2......Eti 'MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZA SABABU ZA KIFO CHA YANGA'.....Yaani Yanga ife kwa kupoteza mechi na Toto Africans na Kagera Sugar!!!!......Ama kwao Clouds timu kushika nafasi ya 3 ni kiashiria cha kushuka daraja...Yanga ina mechi tatu kumaliza ligi na ikishinda zote inaweza kushika nafasi ya 2....

Shaffih Dauda in Sports.: MTANGAZAJI WA SPORTS XTRA/BAR YA CLOUDS FM/TV ATIMULIWA NA WANACHAMA KWENYE PRESS CONFERENCE YA YANGA!

Shaffih Dauda in Sports.: KAMATI YA TIBAIGANA YAITUPILIA MBALI RUFAA YA YANGA.

Shaffih Dauda in Sports.: OFFICIAL: RUFAA YA YANGA YAPIGWA CHINI !

Shaffih Dauda in Sports.: SIMBA YAZIDI KUCHANUA MAKUCHA NA KUTAMBA KILELENI - YANGA YAPIGWA TENA HUKO KAGERA

Shaffih Dauda in Sports.: MATUKIO YA PICHA UWANJA WA KAITABA YANGA NA KAGERA SUGAR

Shaffih Dauda in Sports.: BAADA YA RUFAA YAO KUTUPWA - YANGA WATAFAKARI CHA KUFANYA

Shaffih Dauda in Sports.: KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART 1

Shaffih Dauda in Sports.: KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART II

Shaffih Dauda in Sports.: KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART III

Shaffih Dauda in Sports.: WASIKILIZE BAKARI MALIMA ' JEMBE ULAYA ' NA MDAU HEAVY D JUU YA YANGA.

Tunajua kwamba mmeamua kuisakama Yanga kwa kujipendekeza TFF ili mpatiwe tenda ya kutengeneza tiketi kwa ajili ya mechi za ligi kuu.....

KAMPUNI NNE ZAPITA TENDA YA TIKETI

Kampuni nne kati ya sita zimepita hatua ya kwanza ya mchakato wa kupata moja itakayofanya kazi ya kutengeneza tiketi za elektroniki kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na nyingine zinazosimamiwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Shughuli ya ufunguzi wa maombi ya hatua ya awali ya kuonesha nia (Expression of Interest) kwa ajili ya tenda hiyo ilifanywa jana (Aprili 19 mwaka huu) na Kamati ya Mipango na Fedha ya TFF ambayo ndiyo Bodi ya Tenda ya shirikisho.

Kampuni ambazo zimepita hatua hiyo ya kwanza sasa zinatakiwa kuwasilisha rasmi tenda zao kwa ajili ya shughuli hiyo ndani ya kipindi cha wiki tatu tangu ulipofanyika ufunguzi wa hatua ya kwanza.

Baadaye Bodi ya Tenda itakutana tena kupitia tenda zitakazokuwa zimewasilishwa na kufanya uteuzi wa kampuni moja itakayofanya kazi hiyo.

Kampuni ambazo zimefanikiwa kuingia katika hatua hiyo ya pili ni CRDB Bank PLC, SKIDATA People Access Inc., Prime Time Promotions na Punchlines (T) Limited.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Yanga: Daima Mbele, Nyuma Mwiko
 
Bala

Yanga wamepoteza dira mtani, kuna viongozi pale wanaongoza yanga kishabiki kama tuko seventies... for Yanga kubadilika lazima waandamwe

wakibembelezwa usitegemee chochote mtani
 
Bala

Yanga wamepoteza dira mtani, kuna viongozi pale wanaongoza yanga kishabiki kama tuko seventies... for Yanga kubadilika lazima waandamwe

wakibembelezwa usitegemee chochote mtani
Suala la tatizo la uongozi ninalijua sana cuz.....Na hata hapa nililieleza

Safi sana Toto Africans na Kagera Sugar....

Kwa hali ilivyo sasa ndani ya Yanga sioni ajabu kufungwa mechi 2 mfululizo...Yanga tumefugwa kwa sababu ya kujitakia....Kiwango cha uchezaji kimeshuka,wachezaji hawana morali ya ushindi......Timu haina nidhamu kuanzia kwa vipngozi,kocha mpaka wachezaji....

Lawama zangu nazielekeza kwa Mwenyekiti Nchunga na viongozi wenzake kwa kitendo chao cha kipuuzi na cha kijinga kabisa cha kumtimua SAM TIMBE ambaye aliwaletea ubingwa wa VPL na KAGAME(kitu ambacho kilimshinda Papic kiasi cha kubwaga manyanga na kuacha kuifundisha Yanga)...Sikuona sababu ya viongozi wa Yanga kumtimua Timbe na kumrudisha Papic ambaye tayari alishindwa kuipa mafanikio Yanga....

Kwa ujumla mpaka dakika hii Yanga hatuna chetu mwaka huu.....Hata nafasi ya 2 sio yetu.....Bingwa mwaka huu ni SIMBA na naomba nitumie fursa hii kuwapongeza watani wangu akina Masuke, PrN Kazi, Crashwize na wanyama wengine kwa kujihakikishia Ubingwa mapema kabla hata ligi haijaisha......Hongereni sana SIMBA....

Yanga tunachotakiwa ni kujipanga na kuangalia ni wapi tumekosea na ikiwezekana kumtimulia mbali Kosta Papoc na magarasa yake Mwape na Asamoah......Ikiwezekana tumrejeshe SAM TIMBE ama tumpatie timu MASTER(Charles Boniface)......

Poleni sana wana Yanga wenzangu kwa kipindi hiki kigumu.....Ni hali ya kawaida katika soka la ushindani...

Yanga: Daima Mbele, Nyuma Mwiko......

Tatizo ni hawa vijana wa Clouds wanaojifanya wajuaji kiasi cha kuonesha mahaba ya waziwazi kwa lengo wanalolijua wao....Wanafikia hata hatua ya kuitabiria Yanga kifo....

Hivi umepata muda wa kuwasikiliza hawa Clouds na mada zao zinazoihusu Yanga?....Wanaiongelea Yanga as if inashika nafasi ya mwisho ama ya 2 toka mwisho.....
 
Kumbe Bala ww Yanga !! Mimi napenda Simba timu ya waarabu...
 
Mtani Balatanda relax, hawa jamaa ndo walivyo timu ikifanya vibaya, ungewasikia siku ile Simba imepigwa tatu na wale waarabu wa Algeria kabla Okwi hajafunga goli lililoipa Simba nafasi ya kusonga mbele kama wewe ni mshabiki wa Simba ungeweza kuzima redio, hata kipindi kile cha timu ya Taifa ilivyopigwa tano Misri huwezi amini kama redio iliyokuwa inatangazwa inafanya biashara na watanzania au imepewa leseni na serikali ya Tanzania, mimi nishawazoea wakianza kutangaza habari ambazo sipendi kuzisikia nahamisha stesheni, Kidogo Ibrahim Masoud huwa anajizuia habari mbaya zinazoihusu Simba nadhan kwa sababu ni Kiongozi lakini waliobaki timu yoyote ikifanya vibaya kama unaishabikia ukiwasikiliza sana unaweza kuihama dawa ni kubadili tu radio stesheni na kutotembelea blog yao mara kwa mara.
 
hao ndio wataalam wa soka tanzania na wasemaji wa tff na wasemaji wa soka la tz na kama umewafuatilia zaidi wakitoa analysis za kukopi tokea goal.com na supersport ndio wanajiona wao ndio kila kitu bongo ngoja tuone..
 
Asante kwa kuniwekea link ya picha za Bukoba
 
Kwa muda mrefu sasa nimeshangazwa na propaganda chafu zinazoenezwa na Shaffih Dauda kupitia blog yake pamoja na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM dhidi ya timu ya Yanga.....Shaffih na wenzake akina Ibrahim Masoud ''Maestro'(ambaye ni kiongozi wa watani zetu Simba) kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiisakama Yanga kupitia blog hiyo na Redio kiasi cha kusema kwamba Yanga inakufa sasa.....

Nataka tu kumwambia Shaffi na wenzake Maestro,Jeff Leya na Alex(Luambano) kwamba pamoja na uzishi na fitna zao Yanga kamwe haitakufa,kutokufanya vizuri mwaka huu si kigezo cha kuitabiria kifo Yanga na akumbuke kwamba Yanga sasa hivi iashika nafasi ya 3 na si ya mwisho wala ya 2 ama 3 kutoka mwishoni sasa iweje awaalike akina Mwaisabula na kuanza kuitabiria Yanga kifo?.....Yanga imeanzishwa mwaka 1935 na bado ipo na itaendelea kuwepo......

Ni upuuzi kuisakama timu ambayo inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi na ambayo bado inaweza hata kushika nafasi ya 2......Msimu wa mwaka 1989 Simba iliponea chupuchupu kushuka daraja katika ligi daraja la kwanza lakini hakuna mtu aliyeitabiria Simba kifo.......Chuki binafsi hazijengi,zinabomoa...

Shaffih na Clouds wanaweza kufanya mambo mengi tu mengine badala ya kutwa kucha kuisakama Yanga kwa sababu tu imepoteza mechi 2......Eti 'MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZA SABABU ZA KIFO CHA YANGA'.....Yaani Yanga ife kwa kupoteza mechi na Toto Africans na Kagera Sugar!!!!......Ama kwao Clouds timu kushika nafasi ya 3 ni kiashiria cha kushuka daraja...Yanga ina mechi tatu kumaliza ligi na ikishinda zote inaweza kushika nafasi ya 2....

Shaffih Dauda in Sports.: MTANGAZAJI WA SPORTS XTRA/BAR YA CLOUDS FM/TV ATIMULIWA NA WANACHAMA KWENYE PRESS CONFERENCE YA YANGA!

Shaffih Dauda in Sports.: KAMATI YA TIBAIGANA YAITUPILIA MBALI RUFAA YA YANGA.

Shaffih Dauda in Sports.: OFFICIAL: RUFAA YA YANGA YAPIGWA CHINI !

Shaffih Dauda in Sports.: SIMBA YAZIDI KUCHANUA MAKUCHA NA KUTAMBA KILELENI - YANGA YAPIGWA TENA HUKO KAGERA

Shaffih Dauda in Sports.: MATUKIO YA PICHA UWANJA WA KAITABA YANGA NA KAGERA SUGAR

Shaffih Dauda in Sports.: BAADA YA RUFAA YAO KUTUPWA - YANGA WATAFAKARI CHA KUFANYA

Shaffih Dauda in Sports.: KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART 1

Shaffih Dauda in Sports.: KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART II

Shaffih Dauda in Sports.: KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART III

Shaffih Dauda in Sports.: WASIKILIZE BAKARI MALIMA ' JEMBE ULAYA ' NA MDAU HEAVY D JUU YA YANGA.

Tunajua kwamba mmeamua kuisakama Yanga kwa kujipendekeza TFF ili mpatiwe tenda ya kutengeneza tiketi kwa ajili ya mechi za ligi kuu.....

Yanga: Daima Mbele, Nyuma Mwiko
Hawa jamaa clouds ni wazandiki sana!
Tena mm nishawapotezea kitambo tuu.
Radio ya kishabiki sana ile kwenye upande wa michezo,imejaa usimba na uazam tupu.
 
Hii nchi kila mtu ni futbol analyst tatizo ni mahala pa kusemea. Ukibahatika kupata pa kusemea kama Shafii na wenzie si haba kwani wavivu wa kusoma wote utawapata. Mwakani utasikia akina Shafii wako kamati ya ligi kisa tu kutoa analysis za uongo na kuwapamba viongozi wa TFF. Muda si mrefu tunakamata namba 200 katika rank za fifa maana usanii haulipi kimataifa
 
Jamani kazi ya waandishi ni kuuarifu uma juu ya kilichotokea kwenye jamii kama tunavoona kwenye stations za walioendelea,angalau kama hujui english pata mfano kutoka bbc swahili,dochivere, sauti ya ujerumani nk.TUkirudi kWa haWA jamaa wa clouds ,wapo tofauti wao Wanafanya kazi kishabiki,na kutoa amri na maelekezo juu ya matukio mbalimbali haswa kwa masrai ya simba ambao wana masrahi nao.
 
Tegete ni mhanga wa hii mijamaa,maskini kosa la kuingia uwanjani amehukumiwa sawasawa na aliyempiga refa wakati adhabu halali ni red card ambayo mhusika anamiss mechi3 bila faini.KAMA clotds wasingepayuka wangetoa adhabu kihakali ,rara hivi wameanyisha kampeni ya kuuondoa uongozi wa yanga madarakani,eti sabb waliwatimua kwenye press conference...NACHUKIA SANA HAWA JAMAA
 
Bala kati ya watu ambao siwezi kusikiliza wakijadili mpira ni hawa watu wa Clouds akina Shafii mpira wao ni wakukopi na kupaste
 
Mimi naipenda Yanga lakini lazima tukubai kwamba Yanga safari hii inaenda kibabaishaji sana! Wewe timu gani inamchezesha mchezaji mwenye kadi nyekundu wakati wanafahamu fika swala halijaamuliwa? Wachezaji wanampiga refa viongozi hawasemi lolote! Na wala hamna hatua zinazochukuliwa. Yanga haina timu ya vijana inashindwa hata na simba. Aibu kwa kweli
 
Back
Top Bottom