Shahada ya kwanza ya Sheria(LL.B) pekee haimfanyi mtu kuwa na sifa ya kuwa Wakili

Asante kwa ufafanuzi, kuna vitu vingi nilikuwa sijivijui kuhusu uwakili na bar examination.
P
 

Chuo kikuu na law school of Tanzania tunafundishwa misingi tu ya kuelewa sheria na maudhui ya sheria tunayofundishwa kule ni 5% tu.
 
Asante kwa ufafanuzi, kuna vitu vingi nilikuwa sijivijui kuhusu uwakili na bar examination.
P
Karibu sana tuendelee kujifunza, mwanasheria ni mwanafunzi wa kudumu. Ukifuatilia threads zangu za sheria kwa karibu utapata maarifa ya kutosha maana tofauti yangu na wapinzani wangu kwenye mijadala ya sheria hapa JF ni kwamba wao wanaongea maneno matupu bila backup ya legal authoritative sources lakini mimi ninaongea with legal authorities kwa maana ya kwamba ninafanya rejea kwenye vifungu au masharti mahususi ya sheria (specific provisions of law), maamuzi ya mahakama (case law) na machapisho mbalimbali ya wanazuoni wa sheria.
 
Weka hivyo vifungu tuone km hana hizo sifa
 
Nyie wanasheria hebu turudi nyuma kidogo, Yule binti mtoto wa Mdee akiwa Bungeni alionyesha wasiwasi kwa waziri wa sheria kupita Bar exam kimizengwe hebu tupeni picha halisi likoje au ni figisufigisu zao za kisiasa?
Kabudi akikataa huo ujinga
 
Sijui hayo mambo lakini nilichomuelewa mleta maada jamaa alitakiwa angalau basi afanye Bar exam
 
Weka hivyo vifungu tuone km hana hizo sifa

SHAHADA YA KWANZA YA SHERIA (LL.B) PEKEE HAIMFANYI MTU KUWA NA SIFA ZA KUWA WAKILI.

Kuna wanasheria na wanasiasa hata raia wa kawaida wanaamini au kuaminishwa kuwa kupata shahada ya kwanza ya sheria (LL.B) pekee inamfanya mtu kuwa na "sifa za kuwa wakili" kwa minajiri ya kuteuliwa ya kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali. Watu wanaounga mkono hoja hii wanasema kuwa Dr. Kilangi alipata shahada ya kwanza ya sheria mwaka 2000 hivyo alikuwa na sifa za kuwa wakili kuanzia mwaka 2000, hii ikiwa na maana kwamba wakati anateuliwa kushika wadhifa wa mwanasheria mkuu tiyari alikuwa na zaidi ya miaka 15 akiwa na sifa za kuwa wakili. Wapinzani wa hoja hii wanasema kuwa Dr. Kilangi alipata sifa za kuwa wakili baada ya kufaulu bar examinations chini ya Baraza la Elimu ya sheria na kuwa wakili mwaka 2011 hivyo bado hajafikisha miaka 15 ya uwakili au ya kuwa na sifa za kuwa wakili. Maoni yangu kuhusu swala la shahada ya kwanza ya sheria kumpa mtu sifa za kuwa wakili ni kama ifuatavyo;

Ibara ya 59 (2) ya katiba imeweka masharti kuwa ili mtu ateulie kuwa mawanasheria mkuu wa serikali lazima awe "wakili" au awe na "sifa za kuwa wakili". Swala la kuwa "wakili" halina utata liko wazi mno na haliitaji mjadala kabisa na swala lenye utata ni mtu mwenye "sifa za kuwa wakili". Mtu mwenye shahada ya kwanza ya sheria hana kabisa "sifa za kuwa wakili" kwa sababu sheria mbili zinataja kwa uwazi mtu mwenye sifa za kuwa wakili katika jamhuri ya muungano wa Tanzania. Sheria zimeweka aina tano (5) za watu wenye sifa za kuwa wakili kama ifuatavyo;


Kwanza, "mtu mwenye Post-Graduate Diploma in Legal Practice" ambayo imetolewa na Law School of Tanzania ana sifa za kuwa wakili, hii ni kwa mujibu wa section 12 (3) of the Law School of Tanzania Act, 2007 (sheria Na. 18 ya 2007). Na mtu kamwe hawezi kupata Post-Graduate Diploma in Legal Practice" ambayo imetolewa na Law School of Tanzania mpaka awe na shahada ya sheria au sifa zingine za kitaalum ambazo zinatambuliwa na Baraza la Elimu ya Sheria (Council for Legal Education), hii ni kwa mujibu wa section 11 (1) (a) and (b) of the Law School of Tanzania Act, 2007

Pili, mtu ambaye ana shahada ya sheria ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki au chuo kikuu chochote ambacho kinatambuliwa na Baraza la Elimu ya Sheria na awe amefauli "Bar examinations" inayosimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria , na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (i) and (b) (i) of the Advocate Act, Cap. 1.

Tatu, Mtu ambaye amekuwa wakili Zanziba, Kenya na Uganda kwa kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya kufanya maombi ya kuwa wakili, na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (i) and (b) (i) of the Advocate Act, Cap. 1.

Nne, mtu ambaye ni wakili wa mahakama zisizokuwa na mipaka ya mamlaka katika maswala ya jinai na madai (court with unlimited civil and criminal jurisdiction) katika nchi za jumuia ya madola au nchi nyingine zilizoteuliwa na waziri wa sheria kwa ajiri hiyo, na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (ii) of the Advocate Act, Cap. 1.

Tano, mtu ambaye ni solisita (solicitor) wa mahakama ya juu ya Uingereza (England), Northern Ireland, Jamhuri ya Ireland na Scotland (United Kingdom).

Hivyo basi, hitimisho langu ni kuwa mtu mwenye shahada ya sheria (LL.B) kamwe hawezi kuwa na sifa za kuwa wakili mpaka apate Post-Graduate Diploma in Legal Practice Kutoka Law School of Tanzania au afaulu mitihani inayosimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria (Council for Legal Education) au awe amekuwa wakili au solisita katika nchi za jumuia ya madola au awe amekuwa wakili katika Kenya, Zanzibar na Uganda kwa kipindi cha miaka mitano.

Yodoki II
 

Hivi mkiishiwa hao wa Post-Graduate Diploma hapo kwanini msiazime mwenye LL.B pekee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…