Mpiga kura, hupiga kura kwenye jimbo alilojiandikisha, iwe ni kura ya Rais, Diwani au Mbunge. Ndio maana siku ya uchaguzi huwa yanabandikwa majina ya wapiga kura, kama jina lako haliko kwenye orodha ya wapiga kura, huwezi kuruhusiwa kupiga kura.
Kama itakumbukwa kuna kipindi nadhani ni miezi ya May/June, NEC ilitangaza wale wote ambao wanataa kuhamisha taarifa zao wafanye hivyo ili zihamishiwe rasmi kule ambako watapigia kura siku ya uchaguzi.
Kwa hiyo whoever anayedhani kwamba atapiga kura ya Rais mahali popote, hiyo ni sawa na kujidanganya.
Niliwahi kusema kwamba serikali ya CCM imesogeza mbele tarehe za kufungua vyuo vya elimu ya juu ili kuwavuruga wanafunzi wa elimu ya juu wasipige kura.