Shahidi kesi ya Wema asema bangi ilikutwa jikoni

Shahidi kesi ya Wema asema bangi ilikutwa jikoni

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
index.jpeg


SHAHIDI upande wa serikali kesi ya Wema Sepetu kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya amesema msokoto wa bangi ulikutwa ukiwa kabatini jikoni kwake.

Hayo yamesemwa na ofisa wa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspekta Willy akimweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula.

Inspekta Willy anakumbuka Februari 4, mwaka huu aliitwa na mkuu wake wa kazi na kupewa jukumu la kufanya upekuzi nyumbani kwa Wema Sepetu ambapo aliongozana na maofisa wenzake hadi nyumbani anakoishi huko Ununio jijini Dar es Salaam.

Alisema baada ya kufika nyumbani kwa Wema walimkuta mfanyakazi wake wa ndani wa kike ambaye walimuomba waonane na mjumbe wa shina wa maeneo hayo ambapo baada ya kufanikwa kumwona walimweleza shida yao na kuanza kazi ya uchunguzi ili kutafuta dawa za kulevya.

Aliongeza kwamba baada ya hapo walifanya uchunguzi ndani ya chumba cha wafanyakazi wa ndani wa kike, walikuta msokoto wa bangi uliotumika ndani ya kibiriti na baadaye walijaza hati ya ukamataji, kisha kuondoka na Wema hadi kituo cha polisi.

Aidha shahidi huyo aliiomba mahakama ipokee kielelezo hicho mbele ya Mahakama ambapo wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alipinga kupokelewa kwa hati hiyo, akidai ina mapungufu ya kisheria. Kutokana na mvutano huo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi kesho kwa ajili ya kutoà uamuzi wa kupokea kielelezo hicho ama la.

=======
Wema Sepetu kukamatwa na kuhukumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya
Yaliyojiri katikati ya mchakato wa upelelezi wa kesi ya wema
Wema kukutwa na kesi ya kujibu
Kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kichwa cha habari kinasema msokoto ulikutwa jikoni...
Story yenyewe inasema msokoto ulikutwa chumbani kwa wafanyakazi wa ndani..
Kipi ni kipi?

Yote tisa, kumi ni kwamba ushahidi huo pekee hauwezi kuwa ni uthibitisho kuwa Wema Sepetu alikutwa na msokoto wa bangi au anatumia bangi. Ni wajibu wa polisi kumtafuta mtu aliyeiweka bangi hiyo nyumbani kwa Wema Sepetu.

Katika nyumba yenye watu wazima wasiopungua watano, hata kama ni nyumba ya Multi au Askofu basi tegemea kukuta chochote cha ajabu kama Pombe Kali, Condomu, Sigara, bangi nk, na hauwezi kujua ni nani mhusika kwa hakika.
 
Yaani Bashite kelele zote zile na kutumia pesa za kodi ya wananchi, matokeo ni kumfikisha Wema Sepetu na "Cha ukucha" mahakamani? Sasa huu kama si ulofa ni nini?
 
House girl mla ganja bado anakaa nae ndani! Yaani akitaka kupika anapiga pafu mbili anairudisha jikoni? Yaani hata mama mwenye nyumba hajui harufu ya bhange?

Ila najiuliza unaweza tofautisha vipi mboga ya msusa na msokoto? Huko jikoni tutajuaje labda ilikuwa mboga ya mchana?
 
House girl mla ganja bado anakaa nae ndani! Yaani akitaka kupika anapiga pafu mbili anairudisha jikoni? Yaani hata mama mwenye nyumba hajui harufu ya bhange?

Ila najiuliza unaweza tofautisha vipi mboga ya msusa na msokoto? Huko jikoni tutajuaje labda ilikuwa mboga ya mchana?


Soma vizuri, ni bange iliyotumika, yaani kipisi a.k.a cha ukucha. Huwezi kupika kipisi.
 
Kama shida ni kutumia madawa basi waende vituo vya mabasi kuna mateja kibao wakamatwe na kufunguliwa mashtaka maana mmeshindwa kukamata waingizaji
 
Back
Top Bottom