Nianze kwa kusema, mimi sio mwanasheria ila naijua sheria na nashukuru Mungu amenijalia IQ kubwa sana.
Leo kwenye tovuti ya mwananchi, nimesoma muendelezo wa ushahidi dhidi ya Sabaya, na leo shahidi wa 6, diwani wa CCM alikuwa anatoa ushahidi wake.
Nimeshituka sana baada ya kujua kuwa aliyekuwa anatoa ushahidi ni diwani wa Arusha. Nilijua watu wa Arusha wajanja, mbona wanaongozwa na diwani mjinga kiasi hiki, kwanza hajui hata kupangilia uongo.
Kati ya mambo aliyoyaweka bayana ni :-
1. Kwanza alipigwa nusu ya kufa, mpaka akapoteza fahamu, na kuzinduka baadae...
2. Muda huo huo, alipigwa vibao viwili vya mfululizo, mpaka vikamuathili usikivu wake. Akawa hasikii vizuri.
2. Akachukuliwa na hadi kwa mfanyabiashara aliyekuwa anatafutwa na Sabaya...
Akasikia Sabaya anawaambia walinzi wa ile nyumba, yeye ni DC wa Hai...ametumwa na Magufuli kuwashughulikia waujumu uchumi. (Kumbuka jamaa, muda mfupi alipigwa nusu ya kufa, na vibao vikaziba masikio)
Baada ya kumkosa mfanyabiashara, Sabaya alitoka, Simu yake ikapigiwa, lilikuja jina la DC wa Arusha, Kenan Kihongosi,... ( Huyu aliyepigwa nusu kifo, alionaje Jina la DC Arusha?)
Baadae, Msangi anasema, baada ya mawasiliano yale, Sabaya alisema, Kenan ni maskini, anatumia Altezza.
Hoja nyingine, Msangi anasema, alimsikia Sabaya anasema yeye anamsikiliza Magufuli tu, vikalagosi wengine hawampi shida kabisaa.