Sasa hapo swali gumu ni lipi, very childish.Mkuu,
Mbona hujatuletea Cross Examination baina ya Mawakili upande wa Mtuhumiwa pamoja na Shahidi?
Ukikutana na Mawakili wanaouliza maswali ya kiakili, mashahidi wengine wangekataa kutoa Ushahidi.
Umesema umepigwa karibu na kifo, unaweza kuelezea mahakama hii kifo ni nini? Nusu yake je? Umewahi kufa ukajua kukoje?
Umesema umefungwa miguu na pingu, kweli au si kweli? Miguu yako ina mzunguko kiasi gani? Iweje pingu ya kufungia mikono ikaweza kukufunga Miguu?
Masalia ya Sabaya..Nianze kwa kusema, mimi sio mwanasheria ila naijua sheria na nashukuru Mungu amenijalia IQ kubwa sana.
Leo kwenye tovuti ya mwananchi, nimesoma muendelezo wa ushahidi dhidi ya Sabaya, na leo shahidi wa 6, diwani wa CCM alikuwa anatoa ushahidi wake.
Nimeshituka sana baada ya kujua kuwa aliyekuwa anatoa ushahidi ni diwani wa Arusha. Nilijua watu wa Arusha wajanja, mbona wanaongozwa na diwani mjinga kiasi hiki, kwanza hajui hata kupangilia uongo.
Kati ya mambo aliyoyaweka bayana ni :-
1. Kwanza alipigwa nusu ya kufa, mpaka akapoteza fahamu, na kuzinduka baadae...
2. Muda huo huo, alipigwa vibao viwili vya mfululizo, mpaka vikamuathili usikivu wake. Akawa hasikii vizuri.
2. Akachukuliwa na hadi kwa mfanyabiashara aliyekuwa anatafutwa na Sabaya...
Akasikia Sabaya anawaambia walinzi wa ile nyumba, yeye ni DC wa Hai...ametumwa na Magufuli kuwashughulikia waujumu uchumi. (Kumbuka jamaa, muda mfupi alipigwa nusu ya kufa, na vibao vikaziba masikio)
Baada ya kumkosa mfanyabiashara, Sabaya alitoka, Simu yake ikapigiwa, lilikuja jina la DC wa Arusha, Kenan Kihongosi,... ( Huyu aliyepigwa nusu kifo, alionaje Jina la DC Arusha?)
Baadae, Msangi anasema, baada ya mawasiliano yale, Sabaya alisema, Kenan ni maskini, anatumia Altezza.
Hoja nyingine, Msangi anasema, alimsikia Sabaya anasema yeye anamsikiliza Magufuli tu, vikalagosi wengine hawampi shida kabisaa.
Zipo pingu za plastic zile wanazofungiwa magaidi kule Afghanistan, kiazi wwMkuu,
Mbona hujatuletea Cross Examination baina ya Mawakili upande wa Mtuhumiwa pamoja na Shahidi?
Ukikutana na Mawakili wanaouliza maswali ya kiakili, mashahidi wengine wangekataa kutoa Ushahidi.
Umesema umepigwa karibu na kifo, unaweza kuelezea mahakama hii kifo ni nini? Nusu yake je? Umewahi kufa ukajua kukoje?
Umesema umefungwa miguu na pingu, kweli au si kweli? Miguu yako ina mzunguko kiasi gani? Iweje pingu ya kufungia mikono ikaweza kukufunga Miguu?
Hakuna kesi ya kumfunga mbowe paleUsisahau na team upinzani inazidi kukiona cha moto. Wameanza na kaka lao Mbowe kapigwa kesi ya ugaidi, halafu atafungwa miaka ambayo idadi yake haijulikani. Akija kutoka huko ashakuwa zezeta tayari.
Hii nchi hii!!!!
Zilete wewe.Mbona zile za mashaidi kushindwa kutetea ushaidi hamleti
Ni wapuuzi wachache kama wewe wanaoweza kuamini kama pale kuna kesi! uhuni wa hawa jamaa umeshapuuzwa na ndio maana hata majirani zetu wanatucheka kumwita Mbowe GAIDI.Usisahau na team upinzani inazidi kukiona cha moto. Wameanza na kaka lao Mbowe kapigwa kesi ya ugaidi, halafu atafungwa miaka ambayo idadi yake haijulikani. Akija kutoka huko ashakuwa zezeta tayari.
Hii nchi hii!!!!
Shahidi wa sita katika kesi ya Unyang'anyi wa Kutumia Silaha na uporaji inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkaoni Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya(34) na wenzake wawili,Bakari Rahibu Msangi ameieleza Mahakama kuwa kipigo alichokipata ni sawa na nusu kifo kwani alipoteza fahamu kwa muda huku akiwa amefungwa pingu mguuni na mikononi na walinzi wa Sabaya walimwambia kosa ni kuingilia dili ya Mkuu wao na sijui kama anaweza kubaki salama.
Sabaya na wenzake Silyvester Nyengu(26) na Daniel Mbura(38) wanatuhumiwa Kutumia Silaha kupora kiasi hicho cha pesa na Mali katika tukio lililotokea Februari 9 mwaka huu katika duka la Shahiid Store lililopo mtaa wa Bondeni Jijini Arusha duka linalomilikiwa na Mfanyabiashara Mohamed Saad Hajirini (45).
Msangi Alisema mungu ndio anajua kipigo alichokipata kutoka kwa walinzi wa Sabaya walivyompigia kwa amri ya Mkuu huyo na kusema tu hadi Sasa hawezi kusikia vizuri kufuatia masikio yake kutosikika vizuri kufuatia makofi mawili ya nguvu ya mfululizo aliyokuwa akipigwa kichwani,masikioni na mwili mzima na hajui kilichomfanya kuzinduka na kuwa hai hadi Sasa.
Alisema mlinzi wa Sabaya alimwambia Msangi kuwa tatizo lake ni kuingilia dili la Mkuu General Lengai Ole Sabaya na kuwa kiherehere kufuatilia mambo yake na salama yake ni yeye kumwonyesha Mohamed Saad Hajirini au Ally Saad Hajirini alipo vinginevyo hatabaki salama kwani anaweza kuuawa.
Shahidi Alisema hayo wakati akiongozwa na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali,Tumaini Kweka Mbele ya Hakimu Mwandamizi,Odira Amworo na kusema kuwa wafanyabiashara hao wa kiaarabu walitafutwa na Sabaya usiku kucha hadi majumbani mwao lakini hawakuweza kufanikiwa kuwapata usiku huu hadi walipoamua kukataa tamaa.
Alisema wakati anazungushwa mjini maeneo mbalimbali kuwasaka akina Hajirini,Sabaya aliendelea kumtisha kwa Bastola akiwa ndani ya gari na aliomba kutouawawa kwa kuwa ana Mke na watoto ambao wote ni wagonjwa na hana shida yoyote na Sabaya lakini alisisitizwa kuhakikisha anawaonyesha Waarabu ili aweze kusalimika.
Msangi ambaye alikuwa akitoa ushahidi huku akilia kwa uchungu aliendelea kusema kuwa alimsikia Sabaya akisema kuwa shughuli zote anazifanya Arusha za kuwasaka Waarabu ni maelekezo kutoka ngazi ya juu hivyo hakuna kiongozi wa Arusha wala Polisi anayeweza kumuuliza chochote pindi anavyofanya shughuli Arusha.
Alisema na kumsikia Sabaya akitaka Derava amweleza Msangi kuwa mie napata maelekezo kutoka kwa mtu mmoja tu wa nchi hii ya Tanzania( alimtaja Marehemu Dk John Magufuli) na sio mtu mwingine yoyote hivyo usiwe na kiherehere cha kufuata katika mambo yake na akimwona akae mbali kabisa.
Shahidi Alisema Sabaya akimtafuta Mohamed Saad Hajirini hadi nyumbani na kwenye gari alibaki yeye na dereva na baada ya muda alisikia ukunga ukitoka katika nyumba ya Hajirini iliyopo katika majengo ya NHC yaliyopo eneo la Makao Mapya Jiiini Arusha.
Alisema ghafla aliona Sabaya na walinzi wake wakirudi katika magari lakini hawakuweza kumpata Hajirini na waliendelea kulalamika kukosekana kwa Mfanyabiashara huyo ila waliapa kumtia nguvuni na wakimpata cha moto atakiona màana anafanya biashara haramu na kuihujumu Nchi.
Msangi aliendelea kuieleza Mahakama kuwa mmoja wa walinzi wake anaitwa Andwer na dereva walioneiana kumsaidia na kumpa mbinu za kuwasiliana na Ndugu au rafiki na alifanya hivyo kwa kupewa simu na alimpigia Mke wake na alikwenda eneo walipo ndani ya muda wa nusu saa na alipofika alimwomba Sabaya kumsamehe mume wake lakini aliishia kutaka kupigwa Risasi ya kichwa.
Alisema bàadhi ya walinzi wa Sabaya walionyesha nia ya kumsaidia lakini walikuwa wakifanya kwa usiri mkubwa kwani miongoni mwao alikuwa anawajua na walimwaahidi kumsaidia Ila awe mtulivu kwa kuwa Mkuu wao alikuwa amelewa hivyo asiwe na papara.
Mwisho
View attachment 1871789
Ni kweli hakuna kesi. Lkn kufungwa atafugwa. Nadhani unakumbuka mashekhe wamekaa miaka 9 gerezani pamoja na kwamba hawakuwa na kesi.Ni wapuuzi wachache kama wewe wanaoweza kuamini kama pale kuna kesi! uhuni wa hawa jamaa umeshapuuzwa na ndio maana hata majirani zetu wanatucheka kumwita Mbowe GAIDI.
Duh hii nchi tulishafika pabaya.
Sheria Na. 24 ya mwaka 1966 ya Ulinzi na Usalama wa Taifa, Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU), Katibu Tawala wa Mkoa atasimamia Maagizo ya KUU
1.2 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
- Madaraka yake yanatiririka kutoka kwa Rais kupitia kwa Mkuu wa Mkoa
- Madaraka kwa mujibu wa sheria Na 19 ya 1997 (kumweka mtu kuzuizini masaa 48 mfulilizo)
hahaha huu ugoro ulioandika hapa ndiyo unatokana na hiyo IQ yako kubwa uliyokua nayo???Nianze kwa kusema, mimi sio mwanasheria ila naijua sheria na nashukuru Mungu amenijalia IQ kubwa sana.
Leo kwenye tovuti ya mwananchi, nimesoma muendelezo wa ushahidi dhidi ya Sabaya, na leo shahidi wa 6, diwani wa CCM alikuwa anatoa ushahidi wake.
Nimeshituka sana baada ya kujua kuwa aliyekuwa anatoa ushahidi ni diwani wa Arusha. Nilijua watu wa Arusha wajanja, mbona wanaongozwa na diwani mjinga kiasi hiki, kwanza hajui hata kupangilia uongo.
Kati ya mambo aliyoyaweka bayana ni :-
1. Kwanza alipigwa nusu ya kufa, mpaka akapoteza fahamu, na kuzinduka baadae...
2. Muda huo huo, alipigwa vibao viwili vya mfululizo, mpaka vikamuathili usikivu wake. Akawa hasikii vizuri.
2. Akachukuliwa na hadi kwa mfanyabiashara aliyekuwa anatafutwa na Sabaya...
Akasikia Sabaya anawaambia walinzi wa ile nyumba, yeye ni DC wa Hai...ametumwa na Magufuli kuwashughulikia waujumu uchumi. (Kumbuka jamaa, muda mfupi alipigwa nusu ya kufa, na vibao vikaziba masikio)
Baada ya kumkosa mfanyabiashara, Sabaya alitoka, Simu yake ikapigiwa, lilikuja jina la DC wa Arusha, Kenan Kihongosi,... ( Huyu aliyepigwa nusu kifo, alionaje Jina la DC Arusha?)
Baadae, Msangi anasema, baada ya mawasiliano yale, Sabaya alisema, Kenan ni maskini, anatumia Altezza.
Hoja nyingine, Msangi anasema, alimsikia Sabaya anasema yeye anamsikiliza Magufuli tu, vikalagosi wengine hawampi shida kabisaa.
Kuna mlevi mmoja wa maji jana nilimsikia akisema huyu ni mtu wa system kesi itaisha ataachiwa na atapewa Ubalozi wa nchi mojawapo ataenda kuishi uko.Huyu kijana usalama wake ni kubaki jela maisha yote.
huyu hata akifichwa wapi atakwishaKuna mlevi mmoja wa maji jana nilimsikia akisema huyu ni mtu wa system kesi itaisha ataachiwa na atapewa Ubalozi wa nchi mojawapo ataenda kuishi uko.
Tuvute subira tuone mwisho wa kesi.
Kuzimia ni nusu ya kufa jombaMkuu,