Shahidi wangu kagoma kwenda mahakamani

scientificall

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
457
Reaction score
328
Katika kesi inayonikabili baada ya kuendelea hapa mahakama ya mwanzo. Kufikia upande wa shahidi wa utetezi yaani mimi kama mtuhumiwa.
Mbele ya hakimu nlisema ninao mashahidi 2, ambao ni mtu ninaeishi nae na mpaka siku natajwa na mshitaki kuwa aliniona nikimuibia nlikuwa kwangu na ninaeishi nae.

Shahidi wa pili ni jirani wa karibu ambae mshitaki alimuita asubuhi amfungulie mlango baada ya kufungiwa nje usiku.


Shahidi huyu wa pili aligoma kuwa shahidi wa mshitaki kwani alikuwa rafiki wake wa karibu sana lakini walikuja kukwazana na kugombana baada ya mshitaki kutengeneza tukio la kuibiwa na kudai aliniona mimi usiku nikimuibia.

Alihitaji huyo jirani ake awe shahidi wake lakini kutokana na uongo ambao angeenda kuhushahidia jirani ake amegoma na mshitaki aliamua kuhama kabisa na hata kabla ya kesi haijaisha.

Kwa upande wangu nilimtaja huyo jirani ake kama shahidi wangu baada ya kuona mshitaki anaidanganya mahakama kuwa alipiga kelele usiku hakusikika na alifunguliwa mlango usiku ule ule wakati ukweli ni kuwa alifunguliwa mlango asubuhi saa moja na jirani ake huyo.

Nimemuomba jirani ake huyo akantolee ushahidi juu ya mda alomfungulia mlango mshitaki na kutokusikika kwa kelele siku ya kuibiwa lakini amegoma kwa kudai mpaka apatiwe samasi ya kwenda huko.

Je kwa upande wangu naweza kuieleza nini mahakama juu ya kutokufika kwashahidi huyu?
Na ni shahidi muhimu sana kwa upande wangu.

Nawasilisha............
 
Omba samansi kama ni shahidi muhimu, ila kama kuna uwezekano wa kupata shahidi mwingine atakayetolea maelezo jambo lile lile, achana nae, atakuharibia kesi.
 
Ngoja wanasheria waje...
Iko Sheria inayomlazimisha Shahidi Kuja Mahakamani...anapelekewa Summons Na Akisema Uwongo huwa anaweza Kuambiwa Shahidi Mbaya na Akatangazwa...
 
Achana nae huyo, tayari ni hostile.
 
Nenda mahakani ukaombe samansi aitwe na mahakama aje kutoa ushaidi akikataa kuitikia wito wa mahakama anaweza akakamatwe kwa kuidharau mahakama Fanya hivyo itakusaidia
 
shahidi amekwisha turn HOSTILE, unachotakiwa ni kuomba mahakama imwite kwa sammons kama shahidi wako. ila kama atafika mahakamani kwa sammons hiyo halaf akakugeuka (akawatoa ushahidi kumsaidia aliyekushtaki) wewe huna budi kumcross examini huyo shahidi mana tayar ameshakugeuka hata kuwa shahid wako tena.
 

ACHENI KULISHA WATU MATANGO PORI..!

A hostile witness, otherwise known as an adverse witness or an unfavorablewitness, is a witness at trial whosetestimony on direct examination is either openly antagonistic or appears to be contrary to the legal position of the party who called the witness.
 
Tofauti ya hiki kingereza chako na maelezo ya hao unaosema wanalisha matango pori ni ipi?
 
Tofauti ya hiki kingereza chako na maelezo ya hao unaosema wanalisha matango pori ni ipi?
Hostile ni pale anapotoa ushahidi dhidi ya alimuita mahakamani ,huyu wa hapa hajimgeuka aliyemuita bdo hajaenda mahakamani kagoma,hawezi kuwa hostile.Kumuita hostile nin,to put the cart before the horse.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…