Shairi: Chombo chenda mrama

Shairi: Chombo chenda mrama

Parasite

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
613
Reaction score
575
kama elimu bahari, makasia yako wapi?
jahazi za kifahari, dereva twapata wapi?
ataendesha kwa shari, kweli tutafika wapi?
bahari ikitulia, chombo kitarudi pwani.

mengi majahazi yapo, kwa majina yao kata.
vifaa vingi havipo, maabara makitaba.
wakufunzi nao wapo, wanakimbia ukata.
bahari ikitulia, chombo kitarudi pwani.

dereva kuangaliwa, kwa jicho la umakini.
vifaa kuagiziwa, maabara za makini.
ndipo mtashangiliwa, kwahiyo yenu yakini.
bahari ikitulia,chombo kitarudi pwani.

nawe abiria chunga,safari unayokwenda.
usiwe kama masunga,mwisho ukashindwa kwenda.
usimkere mchunga,kiuno funga mkanda.
bahari ikitulia chombo kitarudi pwani.

zipo meli na maboti,za injini na umeme.
madereva kwa madoti,maabara za umeme.
tufanyeni utafiti,kwanini wao wanene?
bahari ikitulia chombo kitarudi pwani.


Usiwe kama kasuku,kuiga kila mlio.
Toa lako dukuduku,hata kama kwa kilio.
Elimu bila ya buku,wapi letu kimbilio?
Bahari ikitulia,chombo kitarudi pwani.

Kila kitu kusheheni,unategemea nini?
Wao wanapata wani,ziro kamwe huzioni.
Usiulize kwanini,jibu unalo kichwani.
Bahari ikitulia,chombo kitarudi pwani.
images (1).jpeg
 
Back
Top Bottom