ramadhani kimweri
Senior Member
- Apr 22, 2016
- 181
- 179
HAKUNA TENA SIRI.
Kuna mambo siku hizi, hupayukwa hadharani
Tena mambo ya kishenzi, asoweza firauni
Kila kitu waziwazi, wanotenda faraghani
Wapendanao vizuri, hawapayuki njiani..
Zama zimeshachafuka, mambo ni mitandaoni
Yapaswayo kufichika, yametoka paziani
Watu wanafurahika, dunia ikiganjani
Na hakuka tena siri, mambo yote hadharani..
Watu wanaonyeshana, matendo yao ya siri
Tena aibu hawana, kwa hilo kujifaghari
Ati kufurahishana, uovu ulokithiri
Leo hakuna cha siri, vitu vyote jaharani.
Video tupu za ngono, mitandaonu kujaa
Na tena kwa mashindano, hawaogopi fadhaa
Tunaiga kila neno, hata yasiotufaa
Mengine sio mazuri, kuiga tukuacheni..
Mengine tulioiga, aibu hata kusema
Usagaji na ushoga, kawaida hizi zama
Anaepinga mjinga, aonekana wa nyuma
Tena hufanywa dhahiri, kweupe sio gizani..
Sasa kilicho salia, kuomba kwa Rahmani
Atwongoze kwenye njia, ya salama na amani
Na uzao wetu pia, aubariki imani
Watende mema mazuri, ayapendayo Manani..
[emoji2398]Ibn kimweri
Ramadhanikimweri07@gmail.com
Kusoma mashairi mengine bofya
1. Shairi: Usichezee bahati
2. Shairi: Nimezichoka dharau
3. Shairi: Sirudii matapishi
4. Shairi: Itakuwaje nikifa?
5. Shairi: Sina kosa
6. Shairi: Sielewi
7. SHAIRI; Mama Samia
8. Shairi: Binti kurudi shule
9. SHAIRI: Najipa Moyo
10. Ushairi: Undugu ni kufaana
11. Shairi: Kwaherini wenye simu za mchina
Kuna mambo siku hizi, hupayukwa hadharani
Tena mambo ya kishenzi, asoweza firauni
Kila kitu waziwazi, wanotenda faraghani
Wapendanao vizuri, hawapayuki njiani..
Zama zimeshachafuka, mambo ni mitandaoni
Yapaswayo kufichika, yametoka paziani
Watu wanafurahika, dunia ikiganjani
Na hakuka tena siri, mambo yote hadharani..
Watu wanaonyeshana, matendo yao ya siri
Tena aibu hawana, kwa hilo kujifaghari
Ati kufurahishana, uovu ulokithiri
Leo hakuna cha siri, vitu vyote jaharani.
Video tupu za ngono, mitandaonu kujaa
Na tena kwa mashindano, hawaogopi fadhaa
Tunaiga kila neno, hata yasiotufaa
Mengine sio mazuri, kuiga tukuacheni..
Mengine tulioiga, aibu hata kusema
Usagaji na ushoga, kawaida hizi zama
Anaepinga mjinga, aonekana wa nyuma
Tena hufanywa dhahiri, kweupe sio gizani..
Sasa kilicho salia, kuomba kwa Rahmani
Atwongoze kwenye njia, ya salama na amani
Na uzao wetu pia, aubariki imani
Watende mema mazuri, ayapendayo Manani..
[emoji2398]Ibn kimweri
Ramadhanikimweri07@gmail.com
Kusoma mashairi mengine bofya
1. Shairi: Usichezee bahati
2. Shairi: Nimezichoka dharau
3. Shairi: Sirudii matapishi
4. Shairi: Itakuwaje nikifa?
5. Shairi: Sina kosa
6. Shairi: Sielewi
7. SHAIRI; Mama Samia
8. Shairi: Binti kurudi shule
9. SHAIRI: Najipa Moyo
10. Ushairi: Undugu ni kufaana
11. Shairi: Kwaherini wenye simu za mchina