Shairi hisia zitapita

Shairi hisia zitapita

Mbavu mbili

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2011
Posts
1,457
Reaction score
874
HISIA ZITAPITA...
Watuita chakaramu,ardhi yetu asili
Watuvika uharamu,wageni wanowasili
Matendo yao haramu,wamejawa ukatili
Hisia hisia pita,haki itafuatia

Wageuzwa mahadimu,habithi walojasili
Wanachumwa kama ndimu,fikra zao zi batili
Huyu ndiye mwanadamu,mweusi jua hali
Hisia hisia pita,haki itafuatia

Mahabithi wana damu,dhambi kwao wanajali
Kheli zama zamadamu,lijitetea kwa hali
Halafa wanaheshimu,shetani wamfadhili
Hisia hisia pita,haki itafuatia

Najengea ufahamu,sitojivika medali
Siutaki unajimu, zubaa uachwe feli
Maisha haya magumu,watuachia pingili
Hisia hisia pita,haki itafuatia

Wamekalia sanamu,machuta hawana hali
Walamba sukari tamu,makapi kwetu halali
Ewe mwenyezi rahimu,fungua hizi akili
Hisia hisia pita,haki itafuatia

Rugaruga mwanadamu,ajitoa kwa sabili
Ishi yao twafahamu,amerika wamejili
Watuzwa vya hamuhamu,wasahau uasili
Hisia hisia pita,haki itafuatia

Mola aliturehemu,kila kitu cha asili
Wavitwaa mahasimu,walitutesa mashibli
Enzi zile zamadamu,alijikania abushili
Hisia hisia pita,haki itafuatia
 
Back
Top Bottom