Shairi: Itakuwaje nikifa?

Shairi: Itakuwaje nikifa?

ramadhani kimweri

Senior Member
Joined
Apr 22, 2016
Posts
181
Reaction score
179
Shairi: Itakuwaje nikifa?

Kuna mda ninawaza, itakuwa je nikifa,
Maswali najiuliza, nikifikiria kufa,
Naogopa kujikweza, kuzikwepa mbaya sifa.
Nisife kama fulani, kufa bila ya alama.

Nataka nife shujaa, wakupambania haki,
Nataka niache taa, ambayo haizimiki,
Nikifa niache saa, nyakati kuzimiliki,
Niziweke vitabuni, zitumike kila zama..

Nikifa nife kimwili, Niwe hai vitabuni,
Mufukie wangu mwili, niwe nanyi akilini,
Niache alama kweli, yenye tija duniani,
Wanisome mashuleni, wanitaje kwa heshima..

Niandike madiwani, tungo za kila namna,
Nitoe watu gizani, nimulike kila kona,
Niiweke hadharani, elimu lofichikana
Watu wote mubaini, lililo baya na jema..

Nikifa niache mali, kwa familia nyumbani,
Wasije pata dhalili, kuteseka mitaani,
Mana hamtowajali, Nikifa nimasikini,
Niwachie pesa ndani, ili waishi salama..

Nikifa niache pengo, lisiloweza zibika,
Tena mutunge na tungo, na vitabu kuandika,
Muandike na mabango, mandishi yakisomeka,
Baba juma buriani, tutakusoma daima..

[emoji2400]Ibn kimweri ( Baba juma)
Ramadhanikimweri7@gmail.com
Moshi – Kilimanjaro.
TANZANIA.

Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena
 
Back
Top Bottom