SHAIRI
JANGA LA KUBETI
1. Kipo kilio cha wazi, kingine kimefichika
Mfano kuchunwa buzi, huwezi wazi kuweka
Kwetu kama fumanizi, kilio kimetufika
Kubeti nalo ni janga, limeteka watu wengi
2. Kubeti nalo ni janga, limeteka watu wengi
Watu waishiwa mwanga, kama walao milungi
Mwovu katupiga Chenga, tena kwa yetu shilingi

3. Janga sio kwa mmoja, limegusa kila kundi
Unapotaka kuchuja, wengi wetu ni mafundi
Hazina nyingi zavuja, kwa kupoteza Paundi
Kubeti nalo ni janga limeteka watu wengi
4.Wafanyao biashara, Watumishi serikali
Visiwani hata bara, wengi tumelala chali
Ingawaje inakera, bado twaiona dili
Kubeti nalo ni Janga limeteka watu wengi
5. Taasisi watu wake, nazo zimeingiliwa
Watu wafanya makeke, kubeti wamechaguwa
Mtu binafusi yake, nae anasumbuliwa

6. Wengi tumewapoteza, sababu kubwa kubeti
Puresha walizikuza, mwisho zikawataiti
Vijana wanaongoza, kwenye simu wanabeti

7. Ndoa nazo ziko hoi, kubeti chanzo kamili
Vyuoni wasijidai, kubeti kumeshamili
Imeondoka nishai, hofu pia na kujali

8. Ni Kati ya watu mia, moja aweza kupata
Wengine wataumia, kwa kuugonga ukuta
Wazazi twatazamia, mzizi huu kukata

9. Taasisi za kidini, serikali saidia
Bebeni hii huzuni, kizazi kukiokoa
Njia nzuri kuzibuni, majibu kutupatia

10. Beti kumi zinatosha, kufungua maelufu
Na kama nimepotosha, mnichape maradufu
Hujaelewa kausha, usikomenti uchafu
Mungu wetu tuokoe, epusha kilio hiki