G-less Antonopoulos
Member
- Sep 12, 2018
- 34
- 27
1. Habari afikishiwe, miye Mzenji mwenziwe.
Haliendi kwenginiwe, hilo ni langu mwenyewe.
Upesi nikubaliwe, umri tabu isiwe.
"Huyu namtaka mimi, nimrudishe nyumbani"
2. Nina wengi marafiki, wajuzi wa Aisiti (ICT) .
Yeye kwa kummiliki, tutabadilisha cheti.
Sitini ngo itiki, nisimpe gatigati.

3. Urithi wa nyumba yangu, tamuandikia yeye.
Na kila kilicho changu, kitakuwa chake yeye.
Akitaka roho yangu, niradhi apewe yeye.

4. Yote hayo aambiwe, siwezi bila ya yeye.
Nimekumbwa na kiwewe, yote sababu ni yeye.
Ni busara niambiwe, ni chizi miye kwa yeye[emoji1787]

5. Ombi likikubalika, tagawa kwa nyote pesa.
Mji hautakalika, Foro hadi Mambosasa.
Biriani kadhalika, Malti za bakharesa.

Shairi limetungwa na kuandikwa na HMH, Unguja - Zanzibar.