ramadhani kimweri
Senior Member
- Apr 22, 2016
- 181
- 179
KAMWAMBIE NAMPENDA..
Mwambie ninampenda, moyo umemchagua
Ananifanya nakonda, naishi kwa kuugua
Aje nimfanye kinda, moyo upate kutua
Nakutuma kamwambie, vile ninavyompenda.
Amenichanganya kweli, kazivuruga hisia
Taabani sina hali, nashindwa kuvumilia
Mwambie asende mbali, siwezi kusubiria
Fanya hima kamwambie, kama kweli nampenda..
Aje nimpe mapenzi, maana ninayajua
Bila yeye sijiwezi, nitashindwa kupumua
Kamwambie waziwazi, mwambie ataniua
Nenda basi kamwambie, kiukweli nampenda..
Moyo asiudhulumu, yataniua mapenzi
Kamwambie afahamu, siupati usingizi
Najiona sitimamu, ataka niitwe chizi
Ukifika kwamwambie, kuwa mimi nampenda..
Angejua nateseka , kuvumilia mateso
Sio siri ni hakika, naishi kwa manyanyaso
Siwezi hata kucheka, umekunjamana uso
Basi nenda kamwambie, vile ninapata shida..
Sina furaha moyoni, nayachukia maisha
Yote haya hayaoni, anavyonihangaisha
Nilichokosa ni nini, hataki kunisemesha
Nenda wewe kamwambie, si uongo nampenda..
[emoji2398]Ibn kimweri.
Mwambie ninampenda, moyo umemchagua
Ananifanya nakonda, naishi kwa kuugua
Aje nimfanye kinda, moyo upate kutua
Nakutuma kamwambie, vile ninavyompenda.
Amenichanganya kweli, kazivuruga hisia
Taabani sina hali, nashindwa kuvumilia
Mwambie asende mbali, siwezi kusubiria
Fanya hima kamwambie, kama kweli nampenda..
Aje nimpe mapenzi, maana ninayajua
Bila yeye sijiwezi, nitashindwa kupumua
Kamwambie waziwazi, mwambie ataniua
Nenda basi kamwambie, kiukweli nampenda..
Moyo asiudhulumu, yataniua mapenzi
Kamwambie afahamu, siupati usingizi
Najiona sitimamu, ataka niitwe chizi
Ukifika kwamwambie, kuwa mimi nampenda..
Angejua nateseka , kuvumilia mateso
Sio siri ni hakika, naishi kwa manyanyaso
Siwezi hata kucheka, umekunjamana uso
Basi nenda kamwambie, vile ninapata shida..
Sina furaha moyoni, nayachukia maisha
Yote haya hayaoni, anavyonihangaisha
Nilichokosa ni nini, hataki kunisemesha
Nenda wewe kamwambie, si uongo nampenda..
[emoji2398]Ibn kimweri.