Ukweli kwangu kinaya, mazuri sipigi kumbo,
Na wala sioni haya, kunangwa na masombombo,
Nikiyaona mabaya, nitaimba kama wimbo,
Ukweli kwangu kinaya, unisikize mwajimbo,
Bure ukinichukiya, naona mnywa zarambo,
Kweli ni yenye sabaya, hata uitie shombo.
MBONA SASA mabo ni