Shairi kuhusu Mchakato wa Katiba

Shairi kuhusu Mchakato wa Katiba

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Mchakato wa katiba bado unaendele na huu ni ujumbe wangu kwa leo.

1.CCM na UKAWA,mbona mwazidi vutana ?.
Bado mambo hayajawa,mnaanza kamatana.
Mtaweza kutugawa,na nchi mtaichana.
Tusitumie vibaya, mchakato wa katiba.

2.Tujenge katiba njema,ya nchi siyo siasa.
Tuijenge nchi njema,na tuipige msasa.
Mtapo fanya wema,mtadumu kama kasa.

3.Wananchi tunataka,katiba yenye maana.
Wala siyo takataka,na vurugu ziso maana.
Ubabe mkiutaka,mtaipata laana.
Tusitumie vibaya,mchakato wa katiba.

4.Katiba tukiijenga,sote tutaja fadika.
Katiba tusipojenga,sote hatutaja cheka.
Na kama tukijitenga,mataifa yatacheka.
Tusitumie vibaya,mchakato wa katiba.

5.Ubabe kufanyiana,siyo jambo la maana
vitisho kutoleana,ni mwanzo wa kuachana.
Kwa hoja tukishindana,tutakuja kupatana.
Tusitumie vibaya, mchakato wa katiba.

Tumuombe mungu kama watanzania,tupate katiba bila ya mabaya yoyote.
 
Hakuna kuburuzana , Za utumwa kwa bakora.
Ama kauli ya jana , Mtu kumwita m'bara.
Yataka moyo kitana ,kuchana bila ya dira.
Mchakato umevimba ,mkuu ameuchana.

Kilichpo ni kutimba,kula kisicho lazima.
Posho imepata mwamba,yaliwa ikizizima.
Katiba haina mimba ,tumaini limezama.
Twabaki twawatazama ,Mchakato kama kimba.

Mkuu aliutimba, siku ile ike kwanza.
Kasema yungani simba,kanguruma kama mwenza.
Kufumbuwa na kufumba ,Ukawa wakajibanza.
Hawakutaka kutunza ,katiba ilo na vumba.



CCM na majopo ,wanuka wasema vundo.
Wapita kama mapopo ,jioni kwenda malindo
Wameachwa papopapo ,wacheze wao msondo,
Tatu mezua mshindo,MWIBA umechoma ndipo.

Twauita MTAIMBO wazenji wanaujua.
Umenasa tena tambo ,wapita wakiugua.
Bunge lajifanya Tembo, lavuruga likijua
.
Hawana la kujivua ,aibu yao ni wimbo.
 
Napita nikiangaza,wanachotaka kuganga.
Bungeni wajitangaza,ni mambo walishapanga.
Majambo yamewatanza ,warushiana mapanga.
Wamekuwa ni Wamanga.posho itaja waponza.
 
CCM wakutana,wapanga mambo lukuki.
Mambo sio shwari tena ,bungeni hakukaliki.
Kila wanachokinanga ,juu hakitaharuki,
Kamatize zenda mbio ,wapishana kama nyuki.
 
Wallahi narudi shamba ,kuvuna sikudiriki.
Naona watu wembamba,pumzi haziwashuki.
Wengine ka na mimba,kumbe vile mamluki.
Bungeni mambo mkiki, kama kumengia simba.

Wesema bila UKAWA ,mambo watayadiriki.
Kumbe mna popobawa ,jengoni hamkaliki.
Posho wanayopopowa, tena haitamaniki.
Bungeni mambo mkiki ,kama kumengia simba.


Wale waliosaliti,ukawa kuikimbia.
Sasa wavae matiti ,tupate kuwaimbia.
Waje tuwapige miti ,bakora hamsumia.
Na wazitoe sauti ,tuhisi wanaumia.


 
Wapita wakilalama,walobakia bungeni.
Mambo yao si salama, jambo wamelibaini.
Karibu watalihama,shume alala jikoni.
Ile hela mifukoni ,yakumi imeshakwama.

Vumilia kawashinda,wapita wakiropoka.
Sita kama talivunda ,Ndururu tawaponyoka.
Wabunge kama Makinda,macho yameshawatoka.
Posho imeshakauka ,na njaa yaanza winda.
 
Nimezama nimezuka,narudi kwetu nyumbani.
Najua nahitajika ,msimamo si kuhini.
Hapana nimeipaka,bungeni si ukutani.
Wajaribu kujishika ,la sihivyo kaburini
.

Tena nasimama wima,ujumbe kuufikisha.
Kazi mliyotutuma,wachache tumetingisha.
Wingi wao mazima,njia tukawaonyesha.

Akukataae hakwambii toka waona mamboye yamebadilika
Waweza ukae huwezi ondoka.
 
Mchakato wa katiba bado unaendele na huu ni ujumbe wangu kwa leo.

1.CCM na UKAWA,mbona mwazidi vutana ?.
Bado mambo hayajawa,mnaanza kamatana.
Mtaweza kutugawa,na nchi mtaichana.
Tusitumie vibaya, mchakato wa katiba.

2.Tujenge katiba njema,ya nchi siyo siasa.
Tuijenge nchi njema,na tuipige msasa.
Mtapo fanya wema,mtadumu kama kasa.

3.Wananchi tunataka,katiba yenye maana.
Wala siyo takataka,na vurugu ziso maana.
Ubabe mkiutaka,mtaipata laana.
Tusitumie vibaya,mchakato wa katiba.

4.Katiba tukiijenga,sote tutaja fadika.
Katiba tusipojenga,sote hatutaja cheka.
Na kama tukijitenga,mataifa yatacheka.
Tusitumie vibaya,mchakato wa katiba.

5.Ubabe kufanyiana,siyo jambo la maana
vitisho kutoleana,ni mwanzo wa kuachana.
Kwa hoja tukishindana,tutakuja kupatana.
Tusitumie vibaya, mchakato wa katiba.

Tumuombe mungu kama watanzania,tupate katiba bila ya mabaya yoyote.
 
Back
Top Bottom