Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
FREE VOICE
1. Yalipopangwa makundi,
Visebengo walichamba,
Wakazipiga filimbi,
Wamisri ndiyo Mwamba,
Wakazichapa dosari,
Vita mbili yake namba,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea
2. Tuanze gemu ya kwanza,
Vita tukamtoboa,
Ya pili waliomponza,
Mosimane akalia
Tukawa timu ya kwanza ,
Msimamo kukalia,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea
3. Fyokofyoko Majirani,
Mashabiki tukanyimwa,
Kuingia Uwanjani,
Hata wale tulopimwa
Kilichotokea Dimbani,
Tatu bila zimefungwa,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea
4.Kumi zetu Kibindoni,
Tunashika usukani,
Hodi robo mlangoni,
Tuwabebe wajangwani,
Twasogea Sebuleni,
Nne timu shindanoni.
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea
5. Namaliza kwa kusema,
Utopolo tulieni,
Mengi mnayoyasema,
Hayatufuki abadani,
Mungu tumeshamuomba,
Hatutoki kileleni,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea
KAMA SUKARI IKIPANDA CHEMSHIA CHAI
1. Yalipopangwa makundi,
Visebengo walichamba,
Wakazipiga filimbi,
Wamisri ndiyo Mwamba,
Wakazichapa dosari,
Vita mbili yake namba,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea
2. Tuanze gemu ya kwanza,
Vita tukamtoboa,
Ya pili waliomponza,
Mosimane akalia
Tukawa timu ya kwanza ,
Msimamo kukalia,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea
3. Fyokofyoko Majirani,
Mashabiki tukanyimwa,
Kuingia Uwanjani,
Hata wale tulopimwa
Kilichotokea Dimbani,
Tatu bila zimefungwa,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea
4.Kumi zetu Kibindoni,
Tunashika usukani,
Hodi robo mlangoni,
Tuwabebe wajangwani,
Twasogea Sebuleni,
Nne timu shindanoni.
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea
5. Namaliza kwa kusema,
Utopolo tulieni,
Mengi mnayoyasema,
Hayatufuki abadani,
Mungu tumeshamuomba,
Hatutoki kileleni,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea
KAMA SUKARI IKIPANDA CHEMSHIA CHAI