Shairi: Kumi zetu Kibindoni, Tunashika usukani

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
FREE VOICE

1. Yalipopangwa makundi,
Visebengo walichamba,
Wakazipiga filimbi,
Wamisri ndiyo Mwamba,
Wakazichapa dosari,
Vita mbili yake namba,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea

2. Tuanze gemu ya kwanza,
Vita tukamtoboa,
Ya pili waliomponza,
Mosimane akalia
Tukawa timu ya kwanza ,
Msimamo kukalia,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea

3. Fyokofyoko Majirani,
Mashabiki tukanyimwa,
Kuingia Uwanjani,
Hata wale tulopimwa
Kilichotokea Dimbani,
Tatu bila zimefungwa,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea

4.Kumi zetu Kibindoni,
Tunashika usukani,
Hodi robo mlangoni,
Tuwabebe wajangwani,
Twasogea Sebuleni,
Nne timu shindanoni.
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea

5. Namaliza kwa kusema,
Utopolo tulieni,
Mengi mnayoyasema,
Hayatufuki abadani,
Mungu tumeshamuomba,
Hatutoki kileleni,
Waulize watabiri,
Kipi kimewatokea

KAMA SUKARI IKIPANDA CHEMSHIA CHAI
 
Kutokuwafunga wale vibonde kule kwao, bado kunatuweka wakat mgumu...

Ile mechi ilikuwa muhimu saana, kwanza ingeamua sisi kufuzu kwa kushika usukani, jambo ambalo ni zuri zaidi, hatua inayofata tungekutana na maji yetu, ila tukifuzu watu wa pili, robo fainali tutaangukia kwa mamelodi, esperence ama wydad casablanca aisee.. Hawa sio watu wazuri kabisa..

Pili mpaka sasa hatujafuzu, tutegemee mechi ngumu mnoo kutoka kwa as vita, vita watakuja kichwa, miguu, mikono, kila kitu yaani wazima wazima, hawana cha kupoteza na mpira hauna adabu unaweza ukapigwa kimoja, ikawa chomoa, chomoa na ww.

Yote kwa yote kila la kheri chama langu
 
Mtapigwa kimoja tu na AS Vita hamtachomoa mimba ya albino hiyo ukichomoa unaondoka nayo
 
Kwa Simba hii hata aje nani atakaa tu,akuna namna timu itajayokutana na Simba ikaachwa kufungwa, ponea ponea labda wapate droo.
Ao Esperance,Mamelody kwa Simba hii ni wepesi zaidi kuliko unavyofikiri.

Kama ni Esperance walete.

Kama ni Waidad walete.

Kama ni Mamelody walete.

Wape salam waambie Simba ina ukuta wa Belin aujawai tikiswa na yeyote yule,sio bingwa mtetezi Al Ahly wala bingwa wa zamani As Vita.
 
N kweli Ile mechi ya El merreck ilikuwa yakushinda kule kwao ili tumalize on top tumkwepe mamelod
 
waulize watabili
kipi kimewatokea 😁😁😁mbavu zangu jaman
 
Ni sahihi kabisa ulichoongea, game za uhakika zilikuwa za El Merek, huyu alipaswa kufungwa nje ndani na Simba Hadi Sasa angekuwa ameishafuzu Robi fainali. Ila msimamo ulivyo chochote kinaweza tokea, Simba sc Hana 100% kusonga mbele Hadi mechi ya As Vita kwa Mkapa ipigwe. Hivyo Simba sc wasibweteke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…