Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
SHAIRI: KWANINI TWAKICHAFUA KIOO?
MTUNZI: MULIKUZA PASCHAL
Mara nyingi huwa hakidanganyi kile kionacho,
Huonyesha taswira iliyopo mbele yake bila mficho,
Haijalishi taswira ina muonekano gani kwa ya watu macho,
Bali husema na wote wema na wabaya kwa kikioonacho.
Kwa kuwa twakipenda yatupasa tukilinde,
Ndiyo sauti yetu wanajamii katika kila upande,
Wengine hukichukia na kutamani kukivunja vipande vipande,
Lakini husimama imara kama askari mwenye mshale na upinde.
Maharamia nao hawaishi kuharibu kazi zao,
Hupenda kula na kuvuna mazao ya wenzao,
Huwanyonya kama kupe bila kujali hisia zao,
Wengine hutaka kitu kidogo ili wawasambazie kazi zao.
Ni kweli pia mna umoja wenu,
Lakini kila mmoja wenu anatambua haki zenu?
Ni sharti kwenu nyote nyinyi kujiandikisha mpate hakizenu,
Elimu zaidi yahitajika katika jamii kupinga ubatili wa kazi zenu.
Wadhamini mpunguze zenu kashi kashi,
Siyo lazima waseme mtakayo kwani hupunguza yao marashi,
Yahitajika tupate yao mawazo huru yasiyo na bakshishi,
Wasanii wetu wote hawa ndiyo nguzo imara yenye ushawishi.
Tujitambue na sisi kwa tuimbayo na tuigizayo,
Tuweze kuwa walimu bora katika jamii na si vinginevyo,
Kwa kuwa sisi ni kioo yatupasa tuwe nadhifu mbele yao,
Tusipende kuandikwa hovyo magazetini hututia doa machoni mwao.
Mvumilivu siku zote hula mbivu,
Kwa wasanii wachanga ipo siku mtatoka kwenye maumivu,
Tufanye kazi zetu kwa bidii tuache kinyongo na wivu,
Kwa mliopata nafasi mjitume zaidi kuepuka uvivu.