Fikiri nimefikiri, utamu nikabaini,Fikiri ukila mbuzi, nyunyiza na pilipili
Fikiri wake mchuzi, ndimu weka ya ukali
Fikiri simtie nazi , itaharibu misuli
Fikiri akigoma mbuzi, itumie four wheeli
Fikiri nimefikiri, utamu nikabaini,
Fikiri bila kariri, nikaingia rahani,
Fikiri kanipa hari, Iddi ikawa tamuni,
Fikira kwa kufikiri, Utamu ndani kwa ndani.
Fikiri, fikiri, fikiri
Fikiri nawasilim
Fikiri karibuni chai
Mbuzi hakufikiri, Kisu 'kapita shingoni,Na sasa nimefikiri, mbuzi nishamgundua
Na bado ninafikiri, wapi ulimpatia?
Ninazidi kufikiri , mwenyewe aliridhia?
Sitoacha kufikiri, sio wangu alikuwa?
Mbuzi hakufikiri, Kisu 'kapita shingoni,
Kabla hajakariri, Damu katoka shingoni,
Kabla hajatayari, Nyamaye kenda jikoni,
Likuwa mbuzi wa Iddi, Zawadi nililetewa.
hehehehehe hivi umefichwa na nani?acha nifikiri.
Dah! sasa nani alikwambia uludi bongo bana? au ile viza ya botswana iliisha? au hukufikiria?Duh, kloro wala sijafichwa,Fikiria tu Ngeleja anatembelea mtaa wenu,Kila siku saa 12 hadi saa tano usiku,Fikiria pale Internet Cafe wamepandisha bei,Saa moja 3000/= , si anatumia Jenereta...Fikiria mtaji wangu wa Ice cream umekatika woteDuh, acha tu, Vipi huko jamani, wife hajajifungua,Nije kufua nepi, nipate walau ya Cafe tu?Hebu nifikirie, Fikirie.
Dah! sasa nani alikwambia uludi bongo bana? au ile viza ya botswana iliisha? au hukufikiria?
Waifu kenda kusalimia wazazi wewe njoo tu wala usihofu, mimi ni katika wateule wanaume waaminifu wachache sana waliobakia kwenye hii sayari.