Abdallah Masoudi
Member
- May 6, 2019
- 9
- 4
Nipo Mbali:
Nipo mbali unajua,
Simu ndo kiunganishi,
Kwa nilicho kigundua,
Kukuwaza hakuniishi.
Najua unalijua,
Mwanamke ni stara,
Usije jishebedua,
Samaki msafi ukimpara.
Sio tu umevua,
Ukamtia jikoni,
Tumbo litakusumbua,
Usipende uhisani.
Nipo mbali ila hai,
Nitarudi hivi punde,
Ilinde yako nishai,
Isitolewe kwa punje.
Nipo mbali unajua,
Simu ndo kiunganishi,
Kwa nilicho kigundua,
Kukuwaza hakuniishi.
Najua unalijua,
Mwanamke ni stara,
Usije jishebedua,
Samaki msafi ukimpara.
Sio tu umevua,
Ukamtia jikoni,
Tumbo litakusumbua,
Usipende uhisani.
Nipo mbali ila hai,
Nitarudi hivi punde,
Ilinde yako nishai,
Isitolewe kwa punje.