USIPOMSIFIA:
Usipomsifia wewe,
Wapo wa kukusaidia,
Tena si kwa mayowe,
Jinale watamwita Dia.
Usiposifia chochote,
Umeshawapa ushindi,
Hata umvishe Pete,
Wanajiita wahindi.
Usipomsifia mkeo,
Unapunguza mapenzi,
Kwanza wavuliwa vyeo,
Wanaveshwa washenzi.
Kwanini usimsifu?
Acha umajinuni,
Mfanye mchangamfu,
Asikuone muhuni.
Kumsifia si kazi,
Hakuitaji gharama,
Ngoja nikuweke wazi,
Sifu epuka lawama.π¨π½βπ¦―π¨π½βπ¦―π¨π½βπ¦―π¨π½βπ¦―π¨π½βπ¦―