Shairi maalumu kwa Mwigulu Nchemba

Shairi maalumu kwa Mwigulu Nchemba

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,741
Kuna mdau mmoja huko Faceebook ameshuka msitari na utenzi huu, nami nikaona si vibaya nikiwashirikisha hapa jamvini tukafaidi wote... soma hapa

MWIGULU NCHEMBA
kKalamu yangu sambamba,
Kwako Mwigulu wa Nchemba,
Na weka wazi na si chemba,
Kama wima nakuchamba.

Umekuwa jinamizi,
kwa siasa kandamizi,
Ukipita ni ushuzi,
Maneno yako upuuzi.

Siasa za kichochezi,
Na makundi ya Kishenzi,
Kazi yako ni mkwezi
Siasa hizi huziwezi.

CHADEMA mwanana
ccm watuhanya,
Demokrasia walibana
Na Arusha tumewachana

Mabomu mliyarusha,
Kuiteketeza Arusha,
Risasi mlizirusha
Uhai Kuukatisha

Mlitoa na vitisho,
Kwa mafumbo na mipasho
Leo mwatoka jasho,
Sijui tuwapeleke josho?

Heko heko kaka Lema,
Arusha tumerindima,
Hiki kishindo cha CHADEMA
Kinana hoi anahema

Ashakum si matusi
Kunitoa kucha haupaswi
Najua wewe ni kirusi
Watanzania umetuasi

Buriani sisiemu,
Hatutakuenzi marehemu
umeuza nchi kwa ukarimu
Maisha yetu umegharimu

Kadi tamati wa tama,
Hapa mwisho nasimama,
CHADEMA nakutakia salama
MABADILIKO NI LAZIMA
 
Kweye huu ubeti, angalia sentensi ya pili, ndiyo kitakachofuata..

Ashakum si matusi
Kunitoa kucha haupaswi
Najua wewe ni kirusi
Watanzania umetuasi
 
Mwigulu mwenzenu kapigwa BAN kwa uchafu wa domo (matusi).
 
Burudani tosha. Yaani nimecheka mpaka mbavu zimeuma! Mtafuteni mtumieni mwenyewe hili shairi limtoe ushuzi!
 
Yeye ni mchumi daraja la kwanza. Inawezekana akasoma asielewe akadhani unamsifia kwa kumwimbia wimbo wa kumbembeleza baada ya kukung'utwa 4.0.
 
Kunawatu wengine watakufa mapema san mtu kutwa anamwaza mwanaume mwenzake pole mkuu.
 
Mkuu mimi sijui jinsia yako ndiyo maana baada ya bandiko lako napata shida sana kukomenti ila kama ni mwanaume tunahasara sana mkuu hizo siyo tabia za wanaume.
 
Mwigulu punguza spidi mkuu kunawatu unafanya wasilale kabisa.
 
CC Mwigulu Nchemba
Nape Nnauye
Tusker bariidi aka Dentist
 
Hizi laana ipo siku zitamfikia Maulana huko aliko..Mwigulu aangalie sana,
 
Pole sana Mjomba Mwigulu Nchemba, una kibarua kizito kuyasafisha Magamba. Wimbo wako wa kubambikiza watu ugaidi haujabamba,Watu wanauliza kiitikio kuhusu Stella Mwampamba...Kwamba wewe na Lowassa mnajuana kwa vilemba au ni hadithi za wimbo wa Solemba? Mheshimiwa Mwigulu, CCM ni kama dampo la tabata, kwani ufisadi,rushwa na vitisho vimejilaza humo na kunata.Watu wanakusema wewe ni kijiko cha kuchotea takataka hizo, chonde chonde usijitafutie matatizo.Gauni lililo mpwaya Mkama, kurijaribu japo kuvaa kichwa, ni sawa na kuamini chuma kitapukutika kwa kuliwa na mchwa, kumbuka binadamu ni kichwa...tafadhari, usidharau kesho yako maana imefichwa.Jiulize ni kwanini wanakutaka ukae mbele wakati vita ni yenu wote? Usipinge kwamba chambo husifiwa siku zote, lakini faida si yake yote. Ngoma ikivuma sana, hupasuka paa, jiulize wewe utapasukaje?...aagh!
 
Yako wapi majigambo, makombora mlorusha?
Ziko wapi zenu tambo, na kejeli za kuchosha?
Yarabi mmepigwa kumbo, pwaa nje ya Arusha,
Yamewakuta waosha, nanyi mwaminywa utumbo.

Zimekoma zenu nyimbo, virago mmefungasha,
Umewanasa ulimbo, Chadema imewachosha,
Mmepakazwa mashombo,mwenye nguvu mmepisha,
Hizi hapa rasharasha, mwakani gharika mambo.

Pole kwa Shonza mrembo, Mwigulu kakutepesha,
Mwampamba umekwama Mombo, Wasira ametupasha,
Fisadi kamkwaa Rambo, magego kayadondosha,
Kaditama ya Arusha, Kinana zamuuma fimbo.
 
Back
Top Bottom