VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Mwanangu leo amenitumia shairi. Ameliita 'shairi mahiri'. Linasomeka:
Tumbo nimezaliwa nawe,
Tumbo usinifanye nipagawe,
Tumbo usiniache mwenyewe,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo mimi nimesoma,
Tumbo nimesaka maisha mema,
Tumbo nimefika utu uzima salama,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo uanafanya nitamani,
Kupata kila kitu maishani,
Hata vile ambavyo haviwezekani,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo unanifanya kuhama,
Kutoka chama hadi chama,
Unanisogeza karibu na karma,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo unanipelekesha,
Usiku kucha nakesha,
Kupanga cha kuchekesha,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo unanipotezea marafiki,
Sasa naonwa mnafiki,
Naimbwa hata kwenye muziki,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo unafanya natengwa,
Na majungu kujengwa,
Nanyimwa hata machungwa,
Tumbo unalidhalilisha.
Sieleweki,
Siaminiki,
Sishauriki,
Tumbo unanidhalilisha.
Mambo ya expansion joints hayo!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Tumbo nimezaliwa nawe,
Tumbo usinifanye nipagawe,
Tumbo usiniache mwenyewe,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo mimi nimesoma,
Tumbo nimesaka maisha mema,
Tumbo nimefika utu uzima salama,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo uanafanya nitamani,
Kupata kila kitu maishani,
Hata vile ambavyo haviwezekani,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo unanifanya kuhama,
Kutoka chama hadi chama,
Unanisogeza karibu na karma,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo unanipelekesha,
Usiku kucha nakesha,
Kupanga cha kuchekesha,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo unanipotezea marafiki,
Sasa naonwa mnafiki,
Naimbwa hata kwenye muziki,
Tumbo unanidhalilisha.
Tumbo unafanya natengwa,
Na majungu kujengwa,
Nanyimwa hata machungwa,
Tumbo unalidhalilisha.
Sieleweki,
Siaminiki,
Sishauriki,
Tumbo unanidhalilisha.
Mambo ya expansion joints hayo!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam