ramadhani kimweri
Senior Member
- Apr 22, 2016
- 181
- 179
MAMA SAMIA.
Asalamu alykumu, mama uhali gani
Pokea yangu salamu, isije anguka chini
Siandiki kulaumu, kukutia hatiani
Yanilazimu kusema, nimetumwa na wanyonge.
Wamenituma niseme, machache nikuambie
Nchi inao ukame, mama yangu nisikie
Kuna shida ya umeme, hilo uliangalie
Hatusemi kulalama, twasema usitutenge.
Kazi za sasa hasara, hazikidhi mahitaji
Hakuna hata ishara, kizuri kukihitaji
Hata wauza kangara, wameikosa mitaji
Na hata walio soma, hakuna kazi za zenge.
Maisha kupanda juu, huzidishi mishahara
Na tutakufa kwa kiu, wenye nguvu hudorora
Mama usitusahau, unyonge una madhara
Wanao twarudi nyuma, tuhurumie wanyonge.
Hakuna tena ajira, kujiajiri ni shida
Kutwa kucha kuzurura, sio kaka sio dada
Mama mwingi wa busara, tupe sie msaada
Uongozi ni hekima, na uchumi uujenge.
Machinga hana thamani, kwa jamii wafanyao
Hufukuzwa masokoni, hawapati marejeo
Mama na hili huoni, unasubiri machweo
Twaishi kama yatima, kila siku ni mazonge.
Vitu vimepanda bei, mafuta unga sabuni
Hata majani ya chai, bei si kama zamani
Mtaani hakufai, hali za watu ni duni
Watoto watu wazima, twaligombania tonge.
Na hatuli tukashiba, ni kuituliza njaa
Kipato chetu ni haba, hakinunui dagaa
Hatumkumbuki baba, lakini alitufaa
Tulikuwa na salama, alitupenda wanyonge.
Nakuombea kwa mungu, mfalume wa dunia
Ayaondoe magugu, pasiwepo na udhia
Akufunike na wingu, usije potea njia
Uongoze kwa hekima, uhurumie wanyonge..
[emoji2398]Ibn kimweri.
Ramadhani Juma Kimweri.
0746328046
Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena
Asalamu alykumu, mama uhali gani
Pokea yangu salamu, isije anguka chini
Siandiki kulaumu, kukutia hatiani
Yanilazimu kusema, nimetumwa na wanyonge.
Wamenituma niseme, machache nikuambie
Nchi inao ukame, mama yangu nisikie
Kuna shida ya umeme, hilo uliangalie
Hatusemi kulalama, twasema usitutenge.
Kazi za sasa hasara, hazikidhi mahitaji
Hakuna hata ishara, kizuri kukihitaji
Hata wauza kangara, wameikosa mitaji
Na hata walio soma, hakuna kazi za zenge.
Maisha kupanda juu, huzidishi mishahara
Na tutakufa kwa kiu, wenye nguvu hudorora
Mama usitusahau, unyonge una madhara
Wanao twarudi nyuma, tuhurumie wanyonge.
Hakuna tena ajira, kujiajiri ni shida
Kutwa kucha kuzurura, sio kaka sio dada
Mama mwingi wa busara, tupe sie msaada
Uongozi ni hekima, na uchumi uujenge.
Machinga hana thamani, kwa jamii wafanyao
Hufukuzwa masokoni, hawapati marejeo
Mama na hili huoni, unasubiri machweo
Twaishi kama yatima, kila siku ni mazonge.
Vitu vimepanda bei, mafuta unga sabuni
Hata majani ya chai, bei si kama zamani
Mtaani hakufai, hali za watu ni duni
Watoto watu wazima, twaligombania tonge.
Na hatuli tukashiba, ni kuituliza njaa
Kipato chetu ni haba, hakinunui dagaa
Hatumkumbuki baba, lakini alitufaa
Tulikuwa na salama, alitupenda wanyonge.
Nakuombea kwa mungu, mfalume wa dunia
Ayaondoe magugu, pasiwepo na udhia
Akufunike na wingu, usije potea njia
Uongoze kwa hekima, uhurumie wanyonge..
[emoji2398]Ibn kimweri.
Ramadhani Juma Kimweri.
0746328046
Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena