Sauti ya nyikani
Member
- Jan 24, 2015
- 29
- 20
WAWATIBU MALARIA KWA DAWA YA USINGIZI.
Mgonjwa wetu wa tanga, twamlilia nyikani.
Na nduguye ni majanga, ni yule wa visiwani.
Madokta wamewapanga, wawili wote wodini.
Wawatibu malaria, kwa dawa ya usingizi.
Hapa pana siri kali, kuwatibu watu hawa.
Mara dozi ziwe mbili, wakasema wenye pawa.
Bila tatu hatulali, wajibu wabeba kawa.
Wawatibu malaria, kwa dawa ya usingizi.
Madokta kwao Dodoma, nyama choma wajilia.
Wengine walishagoma, kutwa kiguu na njia.
Wagonjwa wanakoroma, ndugu zao tunalia.
Wawatibu malaria, kwa dawa ya usingizi.
Eti wagonjwa kulala, madokta washangilia.
Wapongezana kwa hela, ndugu tulizo lipia.
Na wale wa msafala, kwa nje wachungulia.
Wawatibu malaria, kwa dawa ya usingizi.
Kwenye wao mkataba, mpya wanapigania.
Wao wafata kushiba, wagonjwa wanaumia.
Kama si kifo cha baba, haya yasingetokea.
Wawatibu malaria, kwa dawa ya usingizi.
Huku twambwa tusaini, tiba tumeiridhia.
Kule twambwa tugomeni, hiyo tiba si sawia.
Sasa tumfate nani, mbona wanatuhadaa?
Wawatibu malaria, kwa dawa ya usingizi.
Ndugu tutawashitaki, wagonjwa wakiwafia.
Watatulipa malaki, yote waliyotumia.
Ushabiki hatutaki, maisha twapigania.
Wawatibu malaria, kwa dawa ya usingizi.
Mtazamo wangu mlala hoi.
By: Sauti ya nyikani.