SHAIRI: Midege isiyoliwa ( Isiyo Fugika ) Hiyo ni Midege gani?

SHAIRI: Midege isiyoliwa ( Isiyo Fugika ) Hiyo ni Midege gani?

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
MIDEGE ISIYOLIWA HIYO NI MIDEGE GANI?



Midege isiyofugika, hiyo ni midege gani?

Moyo wahangaika,nitapa jibu gani

Mawazo kunifunika, yataniIsha lini

Midege isiyolika, hiyo ni kidege gani ?



Nimeona ndege wengi, tena wa kila rangi

Wana maumbo mengi, na sauti nyingi nyingi

Wenye kuruka kwa wingi, na mikiani vishungi

Midege isiyolika , hiyo ni midege gani ?



Nimefika kumburu, nikawaona kunguru

Nkaona wao wapo huru, walizunguka duru

Wanacheza zegeduru, hawana udhuru

Midege isiyolika, hiyo ni midege gani ?



Nmewaona kasuku , hawa hawaliki

Lakini si kama kuku, bei yao haishikiki

Wanaleta mtafaruku, kwa sauti lukuki

Midege isiyofugika, hiyo ni midege gani ?



Nawajua bata, nikiwaona wanapita

Hao utawapata, si kila mtaa ukipita

Nyie mnaokula bata, utamu gani mwapata!

Midege isiyolika, hiyo ni midege gani ?



Kuna hawa chiriku, wao si kama kasuku

Muulize mama chiku, usimwulize chausiku

Atakwambia njoo huku,nikondoe shauku

Midege isiyolika ,hiyo ni midege gani ?



Nmewakumbuka kanga, niliwaona kwa luhanga

Hawa ni kama wakunga, watamba chini na anga

Wao wamejipanga, kuyakabili majanga

Midege isiyofugika , hiyo ni midege gani ?
 
Back
Top Bottom