Shairi: Nimezichoka dharau

Shairi: Nimezichoka dharau

ramadhani kimweri

Senior Member
Joined
Apr 22, 2016
Posts
181
Reaction score
179
NIMEZICHOKA DHARAU

Ni kheri niende zangu, sababu umenichoka
Wateseka moyo wangu, nimezichoka dhihaka
Wazarau pendo langu, ya nini kutaabika
Japo bado nakupenda, nimezichoka dharau.

Nimechoka kuziona, kebehi, dharau zako
Waona sina maana, thamani yangu haiko
matusi kunitukana, naonekana kicheko
japo bado nakupenda, zimenichosha dharau.

Bora nipate mwingine, nijifosi kumpenda
Atanipenda pengine, na pia akanilinda
na maumivu yapone, niepuke zako shida
Nisahau kukupenda, nifurahi angalau

[emoji2398]Ibn kimweri
ramadhanikimweri07@gmail.com

Kusoma mashairi mengine bofya Shairi: Hakuna siri tena
 
Back
Top Bottom