Shairi: Nitasimama tena

Shairi: Nitasimama tena

KING ASSENGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
928
Reaction score
1,478
Na nitasimama tena, si ndotoni hadharani
Na mtaniona mchana, sio usiku gizani
Mtaona ninayonena, kutoka kwangu kinywani
Na nitasimama tena, si ndotoni hadharani

Kwa akili nayasema, sijawa punguani
Nitakuwa tena chema, hapa hapa Duniani
Uchumi utachachama, kupita kule enzini
Na nitasimama tena, si ndotoni hadharani

Na shazi la marafiki, kumbe wapo tu wawili
Wengine ni wanafiki, shidani mabaradhuli
Najifunza kwenye dhiki, nasimama mkae mbali
Na nitasimama tena, si ndotoni hadharani

Mpenzi niliyekupenda, kumbe nawe ni shetani
Da dhiki umenifunda, japo ninakulaani
Nenda hayawani nenda, hukupenda asilani
Na nitasimama tena, si ndotoni hadharani

Hata kama naugua, kitandani nimelazwa
Haya sikuyachagua, hata niwe nauguzwa
Mola tu namchagua, mfariji wa kutukuzwa
Na nitasimama tena, si ndotoni hadharani

Ninayatamka hakika, peponi na Duniani
Yasikike na marika, nitamkayo kwa imani
Tena nitaimarika, wakuzuia ni nani
Na nitasimama tena, si ndotoni hadharani

@nicksonPA, Mashauri jr Twitter
 
Back
Top Bottom