Kalamu Yangu
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 1,107
- 1,056
SHAIRI: NURU IMESHINDA GIZA
MTUNZI: Kalamu Yangu
Nuru ndogo ya kurunzi, 'meshinda giza totoro,
Tena mbele ya viunzi, vyenye miba na chochoro,
Wameshinda wanagenzi, si zana siyo michoro,
Giza halikuwatisha, bali nguvu kuwatia.
Tuliwaambia mwanzo, kina Siro na wenzake,
Mkajivunia mafunzo, mwajua kipi mshike,
Mkatupa miongozo, eti siku tuumbuke,
Sasa tumeona nuru, giza halina nafasi.
Kina God na wenzake, tunaona rangi zao,
Twaswali na wao wake, twasoma na wana wao,
Tutawafanya wapweke, kwa dhambi za ndugu zao,
Sasa tunajua yupi, aliye na chuki nasi.
Tena wakatuchanganya,kuna waliowafunga.
Tukiwaza mwatukanya, tukisema ni kisanga,
Sasa mmeyafofonya, hata mwende kwa waganga,
Ilikuwa ishe juzi, mkaipeleka kesho.
Upendo tuliowapa, tukadhani watu wema,
Pongezi tulizowapa, twajuta hata kusema,
Kweli tuliwaogopa, leo tunacheza ngoma,
Giza limeshatoweka, tumeona rangi zenu.
Mkawafanyia hila, si maji si chakula,
Sasa mbili bila, kila mkija hola,
Kama Paulo na Sila, si busara ni sala,
Mwamba ameshawashinda, kubalini mliyabananga.
Hatutokomea hapa, tunamtaka Lijenje,
Wale mliowachapa, mtaja kutana nje,
Haki haitomwogopa, Sangaya ama Sizonje,
Mwanga umeshashinda, safari kama yaanza.
Sasa nachowaomba, PGO muisome,
Mwifwate bila kuyumba, si yeyote mtume,
Siyo mambo ya kubumba, michongo kama Mchome,
Najua mwanuniana, kwa aibu mlopata.
Halafu msimchangaye, chifu mkuu Hanganya,
Wala msimdangaye,ana mengi ya kufanya,
Na Saimoni awakanye, msije kutuchanganya,
Giza limetokomea, si mshumaa siyo jua.
Familia za wahanga, na roho za walioteswa,
Msizitie mchanga, wakaji'si kunyanyaswa,
Kama pesa tutachanga, kwa wote walioguswa,
Nuru imeshinda giza, KATIBA MPYA NJIANI.