ramadhani kimweri
Senior Member
- Apr 22, 2016
- 181
- 179
Huenda tulipendana, na sijui ni kwanini
Miaka tuliachana, lakini bado moyoni
Nahisi tunavutana, kwa macho pia ndotoni.
Au ndio mazea, hutesa na kupumbaza
Kutaka kuyarejea, mwenzenu bado nawaza
Sitaki ije tokea, na hata kwa kuteleza
Nishaoa sasa tena, ninaye mke na mwana
Na ananipenda sana, kifupi tunapendana
Sitaki tujegombana, mwisho tukafarakana
Haachi kupiga simu, wala ujumbe kutuma
Najizuia na hamu, japo moyo waniuma
Sema nikate salamu, namuonea huruma..
ibn kimweri.
Ramadhani Juma Kimweri
0746328046.
Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena
Miaka tuliachana, lakini bado moyoni
Nahisi tunavutana, kwa macho pia ndotoni.
Au ndio mazea, hutesa na kupumbaza
Kutaka kuyarejea, mwenzenu bado nawaza
Sitaki ije tokea, na hata kwa kuteleza
Nishaoa sasa tena, ninaye mke na mwana
Na ananipenda sana, kifupi tunapendana
Sitaki tujegombana, mwisho tukafarakana
Haachi kupiga simu, wala ujumbe kutuma
Najizuia na hamu, japo moyo waniuma
Sema nikate salamu, namuonea huruma..
ibn kimweri.
Ramadhani Juma Kimweri
0746328046.
Mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena