Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 893
- 1,021
PANDE ZA TABU NA RAHA
1 Dunia tunayoishi,nayo ina mengi mambo
Shida huwa haziishi, mawio msalagambo
Tuishini kwa ucheshi,hilo ndio kubwa jambo
Na imejazwa dunia, pande za tabu na raha
2 Lililo wako upande, iwe dhiki au raha
Ndivyo hata usipende, yupi apende karaha
Japo Musa si Kalunde, ndizi haiwi tufaha
Na imejazwa dunia, pande za tabu na raha
3 Wapo hao wenye chuki, uwe nacho au huna
Watu hawaepukiki, nyemi yao kukuchuna
Nao wale mamluki, kazi yao ni kununa
Na imejazwa dunia, pande za tabu na raha
Abuuabdillah
Omari Juma Kimweri.
jumaomari5@gmail.com
0744883353
22022022
Moshi Kilimanjaro Tanzania