Shairi:This is Simba

Shairi:This is Simba

JOTO LA MOTO

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
758
Reaction score
555
Simba.jpg

KUTOKA:KWA MSANII JOTO LA MOTO.

Nakuja kuwasilisha,na pongezi kuzitoa.
Msimu umeshakwisha,hesabu zimeshatoa.
Alama zilizotosha, Mnyama kaziopoa.
Sema this is Simba,Mabingwa wa Tanzania.

Hongera kwa Wachezaji,wapenzi na viongozi.
Timu imevaa taji,kwa kufanya yenu kazi.
Sasa yule bwana Haji, tutakoma kwa mapozi.
Sema this is Simba, mabingwa wa Tanzania.

Mliuanza msimu, sasa mmehitimisha
Mmekwishatoka timu,vidume mmeshatisha.
Hata wale mahasimu,ukweli umewatosha.
Sema this is Simba,mabingwa wa Tanzania.

Mbio mwisho mmefika,mavumbi mlitimua.
Mshindi sasa wacheka, vibonde wanaugua.
Mwali mliyemsaka,Msimbazi keshatua.
Sema this is Simba, mabingwa wa Tanzania

Alama zinazotosha, Mnyama umewekeza.
Kichapo ulikishusha,kwa aliye jidekeza.
Ziliwapanda presha,kila timu mkicheza.
Sema this is Simba, Mabingwa wa Tanzania.

Bingwa Simba mmetoka,uwezo umeamua.
vibonde hoi kuchoka, juu juu wapumua.
Mlilitandaza soka,kila timu kufumua.
Sema this is Simba, mabingwa wa Tanzania.

Kuna walochoka sura,kwa mambo kuelemea.
Eti wanaitwa vyura,mwendo wanachechemea.
Wakajifunze mpira,warudi wamesomea.
Sema this is Sima, mabingwa wa Tanzania.

Nitawataja wachache,ubingwa walowezesha.
Walosababisha cheche,vibonde kutepetesha.
Wakajihisi vicheche, Simba ulivyowatisha
Sema this is Simba, mabingwa wa Tanzania.

Kuna mbabe kichuya,mtaalamu wa soka.
aliwachenga maboya,nyavuni akapachika.
Wakaimba hoya hoya, mashabiki walofika.
Sema this is Simba, mabingwa wa Tanzania.

Okwi yule wa Uganda, timu alisaidia.
Alikabidhiwa tenda,kazi tukashuhudia.
Wabongo wakampenda,mambo akazawadia.
Sema this is Simba, mabingwa wa Tanzania.

Sijamsahau Boko,mpira anaujua
Alizitembeza mboko,goli akawatungua.
Hata yule Kamusoko, habari anaijua.
Sema this is Simba, mabingwa wa Tanzania.

Lodi yupo madhubuti,kwa nyavu kufumania.
Mabeki kumdhibiti mateso kawapatia.
Wakampiga mabuti,bado nyavu kafikia.
Sema this is Simba,mabingwa wa Tanzania.

Kapombe mwana Shomari, sio mtu wa mchezo.
Mambo yake ni hatari,anatisha kama chezo.
Ipo juu yake ari,kama moto wa chetezo.
Sema this is Simba, mabingwa wa Tanzania.

Golini yupo Manula,lango alilidhibiti.
Hakuogopa msala, akazuia mashuti.
Kwa wima na kwa kulala,alichunga milingoti.
Sema this is Simba, mabingwa wa Tanzania.

Ngoja hapa niishie,ujumbe nimeutuma.
Mloshindwa msilie,nendeni shule kusoma.
Sio mwende mtulie,mrudi tena na homa.

Msimbazi ni sherehe, msiba upo jangwani.
 
Shairi zuri sana mkuu, keep it up ila hapo kwenye 'this is Simba' ingekua 'hii ni Simba' kwa muktadha wa ushairi wa kiswahili
 
Back
Top Bottom