Shairi: Twaboronga Kiswahili

Joined
Jan 24, 2015
Posts
29
Reaction score
20
TWABORONGA KISWAHILI.

Twajua neno ONESHA, kwa chenye kuonekana.
ONESHA kuwa ONYESHA, hapa ni lugha gongana.
ONYESHA kunyumbulisha, ONYA, ONYO, ONYEANA.
Twajiita waswahili, kiswahili twaboronga.

TWASIKIA kwa SIKIO, lugha yenye burudani.
SIKIO kuwa SHIKIO, tunalishikisha nini?
SHIKIO kwa mnyubuo, SHIKA, SHIKO, SHIKANENI.
Twajiita waswahili, kiswahili twaboronga.

Na MAHARI neno hili, ni pesa ya kuolea.
MAHARI ita MAHALI, wapi tunapanunua.
MAHALI kwa kiswahili, sehemu tunavyojua.
Twajiita waswahili, kiswahili twaboronga.

Tunaitumiaje GA, neno kuliongezea.
KWENDA na kuwa KWENDAGA, au ndio twatohoa?
Mambo hapo zigizaga, lugha twaitia doa.
Twajiita waswahili, kiswahili twaboronga.

Sauti ya nyikani.
+255756429820.
 
Na tunaandikaje kwenye title ya thread, KISWAGILI badala ya kiswahili?
 
Waeza zidisha/ ongeza pia ONYEKA, ONYANA au pia nami nimeboronga kwa zangu dhana Sauti ya nyikani ....!?
 
Last edited by a moderator:
ahsante wetu malenga,wewe kweli muungwana!
ukweli umeulenga,kasoro umezikana!
pongezi kwako kwa sana.
 
Waeza zidisha/ ongeza pia ONYEKA, ONYANA au pia nami nimeboronga kwa zangu dhana Sauti ya nyikani ....!?

Upo sahihi wala hujaboronga. maana kwenye kunyumbulisha waweza kupta maneno zaidi ya sita kwa kutumia mzizi au shina moja la neno.

mfn: Onya, onyo, onyana, onyeana, onyaneni, onyeaneni, onyeka, n.k.
 
Last edited by a moderator:
twendeni kwetu nyumbani,kiswahili utamuni,chakolea ulimini,karibu tukitwangeni,tTUACHE KUKIBORONGA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…