SHAIRI..UKITHAMINI UREMBO MAMBO YATAKWENDA KOMBO
1.Maisha yetu ni fumbo jaribu kufanya jambo.
Unapozeeka umbo, kumbuka kuacha nembo
Dunia hii ulimbo, usije kufanywa chambo.
Ukithamini urembo,Mambo yataenda kombo.
2.Ukithamini urembo, mambo yataenda kombo
Tutakuimbia nyimbo, umeimaliza mbombo
Utakuwa ni makombo, utafungwa kwenye rambo
Ukithamini urembo mambo yataenda kombo
3.Urembo ni niusemao fikiria mara mbili
Sio ufikiriao, usifikiri kimwili
Kubuni kila uchwao, jambo liletalo mali
Ukithamini urembo mambo yataenda kombo
4.Umri waenda kasi, wala sio lelemama
Ukiigiza ubosi, kwenye mali utakwama
Utaukosa ukwasi, kwa kukosa kujinyima
Ukithamini urembo mambo yataenda kombo
5. Urembo ni sitarehe, pia kuchagua kazi
Myaka sitini ushehe, hujawahi fuga mbuzi
Hata kama wewe shehe, kuhani au mjuzi
Ukithamini urembo mambo yatakwenda kombo
6. Hata ukiajiriwa, kumbuka kujiongeza
Ukicheza utaliwa, kwa kuwa na makengeza
Na wewe unayepewa,
Pato dogo wewe kuza
Ukithamini urembo mambo yatakwenda kombo
7. Haujachelewa bado, acha kukata tamaa
Bado kuna embe dodo, lasubiri kuchukua
Macho yako yawe kodo, fursa inakotokea
Ukithamini urembo mambo yatakwenda kombo
8.mimi pia nilidhani, nimechelewa kwa sana
Nimeijenga imani, kuna siku nitavuna
Kila mara ninabuni, jipya la tena na tena
Ukithamini urembo, mambo yatakwenda kombo
9. Ukiwaacha wazee, vijana pigeni kazi
Kwa kazi tusizembee, mbele tusije kuluzi
Bidii tujitolee, tuweze jenga makazi
Ukithamini urembo mambo yatakwenda kombo
10. Mungu atupe uwezo, wa kuishi kwa akili
Tusije penda vya dezo, na pia vitu vya dili
Tutaepuka uozo, tusipokuwa mahili