Shairi: Usichezee bahati

Shairi: Usichezee bahati

ramadhani kimweri

Senior Member
Joined
Apr 22, 2016
Posts
181
Reaction score
179
USICHEZEE BAHATI.

Wewe si mzuri sana, punguza kuniringia
Wazuri nimewaona, sura zao zavutia
Na mengi wewe hauna, ila nimewakimbia
Moyo umekuchagua, kwako nikama bahati..

Wangapi wamenitaka, watukufu wa tabia
Warembo waloumbika, wakiniona hulia
Nawakataa hakika, ni kwako nakimbilia
Moyo wangu waugua, nimekupenda banati..

Nimesema nakupenda, si vyema kuninunia
Wenzako wananiganda, mapenzi kuyalilia
Wewe waleta mapozi, bahati imekujia
Uache kunizingua, usichezee bahati.

Sina nyumba wala mali, ni mbora wa tabia
Ninamapenzi ya kweli, si kwamba najisifia
Ila najua kujali, kutunza kuhudumia
Juu yako kuchagua, sije sema yalaiti..

[emoji2398]Ibn kimweri.

Ramadhanikimweri07@gmail.com

Kusoma mashairi mengine soma Shairi: Hakuna siri tena
 
Back
Top Bottom