Lidafo
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 889
- 1,789
Kwanza salamu hadhira, Hali yenu vipi shwari,
Nataka niwape dira, Mimi nipo juu ya dari,
Japo kuwa Kuna swira, Sitoiogopa hatari,
Nasihitaji ngawira, Isikilizeni habari.
Utawala waparaza, Kama Simba aliye nyikani,
Unyonyaji unaanza, Wakijiita wahisani,
Kumbe wenzetu ndo Kwanza, Wanaipima mizani,
Mtawala embu waza, umepanda nini shambani?.
Tena waja wajifanya, wanahuruma machoni,
Wazoefu kudanyanya,
Watupeleka mtoni,
Kazi yao kutapanya, Ubaya chuki nyoyoni,
Kodi nyingi za kusanywa, Maendeleo sioni.
Ushahidi upo wazi, Wanayofanya Afrika,
Wanatuchoma mandazi, Wanadai wanapika,
Wanachemsha viazi, Wanasema watulisha,
Afrika bila kazi, Uongo hatuwezi fika .
Wao kwao wamekaa, Sisi kwao tunaenda,
Kazi yao kuhadaa, Pia kwao wanajenga,
Ila kama zatufaa, Mtuambie
walengwa,
Basi kama zina tija, Tuende kwa tahadhari.
Tarumbeta wanapiga, Kelele masikioni,
Twaumwa hatuna tiba, Tunajifia njiani,
Sarafu noti waiba, Wamejaza mifukoni,
Wamekula wameshiba , Kimewakifu tumboni.
Mtawala nakupenda, Ndio maana nakueleza,
Toka moja sasa Kenda, matope nina teleza,
Ahadi zako kalenda, Ila mwingi kujieleza,
Chakula sina madenda, Mtaniua jamani.
Shamba letu tumepanda , Alizeti zi juani,
Nao ndege wametanda, Upepo kasi kusini,
Tumebaki njia panda , Twataka yako idhini,
Mtawala ala ala, Chonde chonde kuwa makini.
Kila siku sisi nyuma, Ndege haina rubani,
Tuna Simba anguruma, Ila muoga nyikani,
Tumebaki nyumanyuma, Vifaranga vya bandani,
Mtawala pananuka, Embu tuchome ubani.
Nina mengi kueleza , Kueleza kiundani,
Tatizo tu sina muda, Tanza wengi hayawani,
Tuna mengi kujifunza, Naeleza jukwaani,
Mtawala nauliza , Hili jua hulioni?.
Elimu Afya ndio chanzo , Serikali hizi samba,
Tusije shika mabango, Kwakweli twaisoma namba,
Samaki hataki chambo, Bahari kupwa ni mamba,
Utawala huu wa joka , Tena lilie magamba.
Umeme maji mitambo, Hili halina uchama,
Tanzania mambo jambo, Jasho la vuja kwa kwama,
Mafunzo yangu mgambo, Hii vita si salama,
Sijui nikae kando, Mtoto nisie na mama.
Sekta binafsi majanga, Haki hakuna kabisa,
Wameyashika mapanga, Wanataka kutuzika,
Ukiona mishahara , Utatamani tapika,
Hasira zinanipanda, Ni
Kweli huna taarifa?.
Wanyamapori mbungani, Faru wanatokomea,
Wapo hoi taabani, Hawawezi kuongea,
Wanaiba mpaka nyani, Kweli wametupania,
Hapa tusikubali, Watulipe kwa fidia.
Miundombinu mibovu, Mikoani mambo bado,
Kuna vituo chakavu, Sahau kuhusu mapato,
Taa zing'ae angavu, Ushuru jaza kisado,
Mtawala nauliza , Mamlaka zipo gado?.
Kuna jambo lanikwaza , Kuhusu mifumo yetu,
Tatizo wengi vilaza, Wamejazana hapa kwetu,
Funga fundo kaza kamba, Fukuza wenye cheketu,
Tuipitie mifumo , Teknolojia Ni yetu.
Haki ni kitu msingi, Kupata tawala Bora,
Polisi Jenga misingi, Usalama uwe bora,
Imarisha na ulinzi, Amani sije dorora,
Wachache wala hii ndizi, Kwa tambo na kwa ving'ora.
Mitaa kariakoo, Manzese changanyikeni,
Mateja kisu kwa Koo, Moshi Arusha semeni,
Polisi jamani loh!, Hizi rushwa ziacheni,
Dhamana sio ubishoo, Majeshi haya twendeni.
Maamuzi tukiyatoa, Yawe na tija taifa,
Yasiwe yakubomoa, Yatagharimu maisha,
Hata Kama kukosoa, Sio kwa kugombanisha,
Tuisafishe madoa, Nguo yetu kuing'arisha.
Amani vyombo vya habari, Ni sifa demokrasia,
Japo hali sasa shwari, Hapo hapo ng'ang'ania,
Utawala sio kamari, Mafisadi fatilia,
Bado Ni ndefu safari, Kwani hawaja kwambia?.
Wengi watakupa sifa , Wapate punje mtama,
Kaa na wenye maarifa, Hiyo ndo yako salama,
Tui kamua machicha, Japo wali ni wa jana,
Hivi mwajenga taifa, Au mnajenga chama?.
Sasa nitoe maoni kuhusu, Tunapo yumba,
Tupo karibu kingoni, Tujenge ya kwetu nyumba,
Nakusudia elimu, Tupite chumba kwa chumba,
Tupitie mitaala , Tutenge chuya na pumba.
Kuhusu haki katiba, Turuhusu mchakato,
Tuwaite maswahiba, Watupe mawazo japo,
Tusiwaogope ngariba, Wenye visu panga rato,
Kipi Bora uchomwe mwiba , Au upate utakacho?.
Usifungie habari, Japo chungu Ila kweli,
Kikubwa ni tahadhari, Wakosoe sio kejeli,
Vipi kuhusu bandari, Mapato vivuko feri,
Nasikia wanaiba, Mpaka shirika la reli.
Mashuleni na vyuoni, Kuna mambo ya kufuru,
Kuna rushwa za nguoni, Ili wapate faulu,
Pamegeuzwa sokoni, Wanatozana ushuru,
Ili wawe hatiani, Rekebisha takukuru.
Ufugaji na uvuvi ,hapa Kuna pesa nyingi,
Tufanye nyingi chunguzi, Tutaongeza shilingi,
Mikakati isiwe mingi, Bali iwe ya msingi,
Tujifunze kwa wenzetu, Wamepataje ushindi.
Usalama uongezwe, Mipakani kadhalika,
Maofisini tusicheze, Kazi kuja aribika,
Sauti yapiga zeze, Kila mtu wajibika,
Tukijifanya kengeze, Madhila yatatufika.
Kwenye kilimo angalau, Tunaona sasa mwanga,
Alipo mtu ni dau, Jahazi sitie nanga,
Muwezeshe kwa pilau, Afunge kiuno kamba,
Jahazi atafikisha , Ameshauona mwamba.
Nasisi wananchi, Tusibweteke jamani,
Tukusanye japo mbichi zitaivia njiani,
Tuipande michikichi, Mafuta jaza dukani,
Fedha yataka nidhamu, alietuloga sinani?
Tunataka vya kuiva, Ila wavivu kulima,
Tutazidi kuumizwa, Kwa uvivu wa kupima,
Kazi ndogo jishikiza, Tuanze panda mlima,
Tushike mipini jembe, Tuanze chimba kisima.
Vijana ndio nguvu kazi, Pombe zinatumaliza,
Tayari tunayo ngazi, Kupanda siwe ajiza,
Tuupande huu mnazi, Tararibu twamaliza,
Tusisubiri ajira, Dunia imebadilika.
Jeshi taifa hongera, Kwa kazi mnayofanya,
Mwapeperusha bendera, Dumisheni Usalama,
Boresheni zenu sera, Kabla mwezi kuandama,
Tusijebebwa machela, Kwa kuendekeza uhasama.
Mwisho nitoe kongole, Kwa wa mwanzo na watano,
Harakati polepole, Japo kijani na njano,
Nazo nguvu za vidole, zimetupa japo ngano,
Nayasema kwa upole, Huo ni wangu mtazamo.
Tena natoa hongera, Kwa wasita mapambano,
Katupeleka sawia, Hapa ntatoa mfano,
Utalii ajira pia, Endeleza msimamo,
Fungua fursa na njia, Dumisha na muungano.
Ukishindwa kuelewa, Basi angalia picha,
Kwa papa nyangumi chewa ujumbe wangu fikisha,
Hasira nimelemewa, Nina mengi kufikisha,
Ukitaka kunielewa, Rudia rudia picha.
Sasa nifike tamati, Yangu nimeyafikisha,
Japo sauti ya mbali, Natumai imefika,
Sijayasema kwa Shari, Ni kheri nimeandika,
Nimemaliza tayari ,Naomba kuwasilisha.
Mwandishi: Shafii R. Bakari(lidafo).

Upvote
2