Shairi:- Wote mlio timamu tukutane kwa mchina

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
25,556
Reaction score
25,342
Nalipiga baragumu, wa bara na visiwani,
Sikie pate fahamu, wote mje uwanjani,
Simba wamevaa njumu, mazembe jasho kwapani,
Wote mlio timamu, tukutane kwa mchina.

Tukutane kwa mchina, wote mlio timamu,
Wamejileta mchana, mazembe siwalaumu,
Japo tumepakana, ni kitoweo adimu,
Tukutane kwa mchina, wote mlio timamu.

Kwa mchina ndio jina, ulianza ujamaa, Nyerere sio kambona, mwalimu alitufaa.
Kikwete hakuyabana, mkapa aloanzia.
Tukutane kwa mchina, wote mlio timamu.

====inaendelea====
 
Hatupajui kwa mchina, twapajua kwa Mkapa
Mazembe kesha china, nawajuza mwanayanga wahapa
Watarudi kwa carina, japo ndege wamelipa
Twende kwa Mkapa, sisi twapajua kwa mkapa.
 
Hatupajui kwa mchina, twapajua kwa Mkapa
Mazembe kesha china, nawajuza mwanayanga wahapa
Watarudi kwa carina, japo ndege wamelipa
Twende kwa Mkapa, sisi twapajua kwa mkapa.
Nimeguswa kwenye mboni, maumivuye kichwani, kwa jambo la michezoni,
Nimepanda jukwaani, ngumi nimtwange Joni, mwakiyembe hata soni,
ALOJENGA NI MCHINA, PESA TEKNO NA VIFAA
 
Nimeguswa kwenye mboni, maumivuye kichwani, kwa jambo la michezoni,
Nimepanda jukwaani, ngumi nimtwange Joni, mwakiyembe hata soni,
ALOJENGA NI MCHINA, PESA TEKNO NA VIFAA
Alojenga ni mchina, hilo tupo pamoja
Tekno na karakana, vyote kaleta kwa pamoja
Pesa kwetu kavuna, tena kwa mkopo wa 'haja'
Maumivu yashapewa dawa, kwa jambo la michezoni

Mchina pesa atalipwa, makubaliano yapo sawia
Uwanja wetu mpwa, kwa Mkapa jina sawia
Maji jaa maji kupwa, mchina hana chake sawia
Maumivu yashapewa dawa, kwa jambo la michezoni
 
Mbona mnakejeli, mbwata sauti ya tako!
Kwa jinsi mlivyofeli, yalishindwa matambiko!
Ndipo mkapanda meli, kwenda china si kwa ngoko!
Mti kuitwa jinale, matundaye huhusika.

TUKUTANE KWA MCHINA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…