Shairi: Ziwe mbili au tatu

Shairi: Ziwe mbili au tatu

Ibrambeya

Member
Joined
Jul 25, 2014
Posts
36
Reaction score
2
Ziwe mbili au tatu, Hilo Bado mgogoto,
Nina mengi nawazua, wa kunifumbua hola,
Na hata akitokea, Heko yake nitampa,
Ziwe mbili au tatu; Serikali Tanzania?

Tume yake Warioba, Maoni ilikusanya,
Sampuli ikapata, Wenye hoja dadavua,
Kablasha kurundika, zikaitwa ni Rasimu
Ziwe mbili au tatu; Kwangu Bado ni utata.

Ubishi ukarandama, vikaibuka vihoja,
Ukawa na Tanzania; Mia mbili nae moja,
Midahalo imetanda, kuzimwaga zao fikra,
Ziwe mbili au tatu ; Ndio Msingi Katiba.

Ccm Upinzani, Ninataka Leo jibu,
Haja zenu nasikia, vikao nimeshiriki,
Mlitaja na gharama, na wengine kutengua,
Ziwe mbili au tatu; Pabaya Mtatufikisha.

Wananchi lalamika, usawa ati haupo,
Mara koti Muungano, Kuna mmoja kalivaa,
Ardhi nazo ajira, twadaiwa viparata,
Ziwe mbili au tatu; Changamoto tutanzue.

Wanazuoni kutanda, Midahalo kukamata,
Suluhu kuangazia, njia ipi tuipite,
Raisi akaibuka, hotuba zake katoa,
Ziwe mbili au tatu; Tuzitumie busara.

Kuna moja naliona, nathubutu kulisema,
Tanzania walalama, wasubiri tafuniwa,
Mchakato wa Katiba, tushiriki sisi sote,
Ziwe mbili au tatu; Ndio Roho ya Katiba.

Tusijesemea Ninge, maji yakisha mwagika,
Tunamuda kutanzua, sauti zetu zipaza,
Haijali unakotokea, Ipaze yako sauti,
Ziwe mbili au tatu; Pambana popote pale.

Mwenye jibu nipatie, mimi ubongo utandu,
Nimechoka tapatapa, kwa nyingi kauli mbiu,
Washairi mnijibu, Kijukuu chake Robert,
Ziwe mbili au tatu; Kalamu nimeishiwa!.
 
eeee hongera farther !!! lakin hukujibu malumbano nawe bado umetuweka njiw panda. tafadhari tunaomba utoe suluhisho
 
Manedo @
Bado jipu kutumbuka, madaktari tegemeo,

Wa kulitumbua ninyi, mimi ukungu machoni,

Njia panda iko Kwangu, Jibu nilipate kwenu,

Ziwe mbili au tatu; Jibu Kwangu mgogoto!.
 
Nakupa kongole kwako mshair kwa lako zur shair lenye kila umahir! lakin umetuacha na swal kwamba tatu au mbil ngoja tuumz vchwa jibu tuliweke waz..!!
 
Nakupa kongole kwako mshair kwa lako zur shair lenye kila umahir! lakin umetuacha na swal kwamba tatu au mbil ngoja tuumz vchwa jibu tuliweke waz..!!
 
Rudbway@
Nashkur muungwana, Jibu lako nimepata,
Kujibu Sio sharia; ni busara kutumia,
Basi tusubiri jibu, kwa wengine walowazo,
Ziwe mbili au tatu; Ndugu tunawasubiri!
 
Back
Top Bottom