SHAIRI

SHAIRI

MakaDik

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2019
Posts
239
Reaction score
136
KUPOTEZEA

1.Kupotezea ni neno, rahisi kulitamka
Lakini lina vinono, kulikoni kuwa taka
Linavunja mvutano, huziba palotoboka
Kama una jambo baya, potezea litapita

2. Kama una jambo baya, potezea litapita
Watakuona ni boya, badae hutajajuta
Potezea bila haya, mbele yako utapeta
Kama una jambo baya, potezea litapita

3. Ni sawa na kusamehe, Ni sawa na kuachia
Huleta kusitarehe, Mambo ukipotezea
Wachungaji na mashehe, fundisha kupotezea
Kama una jambo baya potezea litapita

4. Mwenzako amekuchiti, potezea usilie
Dawa yake chapa buti, usije mfwatilie
Mwisho atapiga goti, aomba umpokee
Kama Una jambo baya potezea litapita

5. Akutendae ubaya, penginepo amefungwa
Potezea tunza kaya, vumilia ukitingwa
Sio kwamba utapwaya, Mambo yako yatapangwa
Kama una jambo baya potezea litapita

6. Ubaya naousema, Ule wa mahusiano
Mambo mengi yanakwama, bila ushirikiano
Mdomo mkiachama, mkubali na mavuno
Kama una jambo baya potezea litapita

7.
 
Back
Top Bottom