Shajara ya Madikteta

Marekani imeponea chupuchupu kumpata kiongozi wa aina hiyo akiitwa Donald Trump. Kilichowaokoa Wamarekani ni kwamba ni taifa la wahamiaji wa aina zote waliokimbia nchi zao za asili kwa sababu mbalimbali kubwa likiwa maisha bora ya uhuru na haki. Watu hawa waliotoka kila pembe ya dunia walihakikisha wanaunda taifa lenye misingi imara ya utawala isiyotoa ruhusa kwa umungu-mtu kumea na kuchanua.
 
Hakika uko vizuri upstairs...Kwa nini CCM isinunue watu kama ninyi kuliko kuwapanga Lusinde na Msukuma kumshambulia poti wanngu Prof Muhongo eti kwa kuwa America mawazo tofauti na ya Mwendazake.Bunge waache watu waongee aliyekuwa anaogopwa hayupo...
 
Ukishusha madudu ya jiwe usikose kunitag. 😂
 

Tunasubiri mkuu
 
Dah! Yaani madikteta wanafanana sana! Usisahau kuweka na kisa cha Benito Mussolini..
Benito Amilcare Andrea Mussolini alizaliwa mwaka 1883 na kufariki mwaka 1945. Mwanzoni alikuwa ni mwanamapinduzi ya kijamaa.

Nchi ya Italia ilipoingia kwenye mgogoro wa kisiasa mwaka 1922, Mussolini alisema yeye pekee ndiyo anaweza kutuliza mgogoro huo, na akapewa mamlaka hayo kama Waziri Mkuu.

Taratibu Mussolini alivunja Taasisi zote za kiutawala na kidemokrasia. Kufika mwaka 1925, akawa dikteta kamili maarufu kwa jina la "Il Duce" ("Kiongozi").

Alikuwa na falsafa yake iliyosema " Il Duce ha sempre ragione (Mussolini was always right).

Athari za ufashisti wa Mussolini kwa nchi ya Italia zilikuwa;

1.Baada ya kuwa Waziri Mkuu, Mussolini alipunguza ushawishi wa Mahakama

2.Akapandikiza vyombo vya habari mamluki

3. Alikamata wapinzani wa kisiasa na kuwafunga jela

3. Aliendelea kufanya kazi ndani ya mfumo wa bunge angalau kidogo hadi Januari 1925, wakati alipojitangaza kuwa Dikteta wa Italia

4. Kufuatia mfululizo wa majaribio ya mapinduzi mnamo 1925 na 1926, Mussolini alizidi kushikilia msimamo wake, na kupiga marufuku vyama vya upinzaji

5. Aliwafuta wabunge zaidi ya 100, na kurudisha adhabu ya kifo kwa wapinzani wa kisiasa

6. Kusitishasha uchaguzi wa serikali za mitaa.

7. Wakati wa vita II ya dunia Mussolini alikuwa upande wa Nazi akimuunga mkono Hitler wa Ujerumani.

Kutokana na falsafa yake ya "Mussolini was always right' nchi ya Italia iliathirika sana kiuchumi kiasi kwamba maisha ya wananchi yalikuwa magumu sana.

Tarehe 28 April 1945 Mussolini na mkewe walishikwa karibu na mpaka wa Switzerland wakijaribu kutoroka kwa kuvaa mavazi kama askari wa Nazi.

Lakini wananchi waliwatambua wakawashika na kuwaweka yeye na mkewe kwenye Jiwe maalum na wakapigwa risasi (firing squad) kwenye mji wa Giulino Azaro kisha miili yao ikawekwa Milan na watu wakaipiga mawe.

HITIMISHO:
Magufuli alikuwa anatembea kwenye kivuli cha Benito Mussolini japo namna ya vifo vyao vinatofautiana
 
Hiki kisa cha Mussolini ni sawa na Tanganyika kwa 99% . Asilimia moja ni hivyo vifo vyao .

Odhis *
 
Akija kuandikwa Stalin.

Kuanzia alipotokea.

Alivyopata madaraka.

Uchaguzi wake wa lugha ni jinsi lafudhi ilivyoathiri matamshi.

Kuchagua maeneo ya kukaa.

Mavazi.

Namna ya kutawala.

Jinsi alivyokua akisimika utawala wake.

Mwisho wake.

Mtasema anafanana kwa 80% na kiongozi kutoka nchi mojawapo ya Afrika
 
Madikteta wote wanafanana KILA kitu.Madikteta wote upokea nguvu toka kwa lucifer kwa makubaliano ya damu na madaraka.Lucifer uwapa madaraka madikteta nao umpa damu lucifer kupitia kafara za watu.Thus madikteta wote wananuka damu za watu,hakuna dikteta mwenye mkono safi.Madikteta wote ni zao la shetani kupitia watoto wa kijini na dikteta upatikana pale jini anapozini na binadamu na kuipuliza pumzi ya kishetani badala ya pumzi ya roho ya Mungu (Jehovah) thus madikteta wote huwa na mfanano sawa wa kuwa na roho ya kishetani ndani mwao.Madikteta wote sifa mfanano ni wauaji,wazinzi,wachawi, mafisadi, upenda kusifiwa kuimbiwa kuitwa mtukufu, Hakuna dikteta yeyeto duniani amewahi shugulika na maendeleo ya watu,wote ufanya vya kuwapa utukufu wao.Wasomi na matajiri ndio wahanga wakuu wa madikteta wote na ndilo kundi linaloshughulikiwa haswa na dikteta sababu ya fear of unknown kuamini ya kwamba linaweza tishia usalama wa Utawala wake.Mdikteta wote wamewekeza kwenye propaganda zaidi kuliko hali halisi huku ofisi zao zikiwa kwenye camera zaidi.Madikteta wote uwapenda wanyonge futureless people maana hili kundi ni rahisi Sana kuwaproganda sababu ya ukosefu wa elimu,ujifanya kuwapenda masikini lakini kwa lengo kuu ni kuwatumia kisiasa zaidi na kupata ulinzi wa uungwaji mkono kwenye chaguzi.Hakuna dikteta anaependa watu zote zile ni camouflage tu.
 
Trump ndie mtawala bogus kuliko wote wa USA na alipewa tu kwa sababu USA bado haijawa tayari kutawaliwa na mwanamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…